TAMASHA la Jambo Fashion Affair linatarajia kufanyika leo Jijini hapa na kushirikisha wabunifu wa ndani pamoja na wasanii kutoka Jijini Arusha na mikoa mbalimbali.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo linafanyika leo, Augustine Namfua ambaye ni Mwenyekiti wa Jambo Festval alisema wamaejiandaa vizuri kuhakikisha wananchi wataohudhuria wanapata burudani ya ubunifu wa mavazi sambamba na muziki.
Alisema wabunifu mbalimbali watakuwepo kama An Nisa, Fatma Naeem, Martin Kadinda ,Wanyoke Lewis, iheartz Collection, Ankara By Chimzy, Fabilouskitenge, Zakia Collection, gLushaju Clothing, Florinyah Designs ,Martin Mukiwa na wengine ambao wataonyesha aina mbalimbali za mavazi.
Namfua alitumia nafasi hiyo kuwasihi watanzania hususan wakazi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo linafanyika leo Viwanja vya Allliance Franc’aise Arusha na kiingilio kikiwa ni h, 20,000 kwa kila mtu.
“Tamasha hili tunalifanya kwa mara ya nne na wasanii mbalimbali pamoja na wabunifu wa mavazi wataonyesha ubunifu wao katika tamasha hili hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kwani mbali na maonyesho ya mavazi pia kutakuwa na burudani za aina mbalimbali sambamba na vinywaji”.
Naye Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd, Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo ndio wadhamini wa tamasha hilo na pia watatoa huduma mbalimbali za vinywaji ili kufanikisha tamasha la ubiifu huku Mkurugenzi wa Alliance Francaise kutoka Arusha, Ga’’ele Lapostolle akisema taasisi yao imeamua kushirikiana na wahusika wa tamasha hilo ili kukuza utamaduni wa watanzania sambamba na ubunifu wa mavazi pamoja na muziki ambao ni ajira kwa vijana.
Naye mmoja kati ya wanamuziki kutoka Jijini arusha ambaye atashiriki katika tamasha hilo na kukonga nyoyo za washiriki wa tamasha hilo, Elisha Simon maarufu kama Hisia aliwasihi wakazi wa Ausha kujitokeza kwa wingi kuona vipaji vya wasanii pamoja na mavazi yatakayoonyeshwa katika tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment