ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 8, 2015

TUNAHITAJI RAIS AWAMU YA TANO AWE MZALENDO SIO MSAKA TONGE

Ningependa kutoa maoni kidogo kuhusu mjadala na mchakato inayoendelea . hivi sasa tunashuhudia watangaza nia wengi wakitangaza nia kwa kutoa hotuba moto moto za kushawishi wananchi wachaguliwe. Nimependa dialogue inayoendelea kuhusu Hotuba nzuri/na kutenda ukishachaguliwa. bahati nzuri kwenye maeneo yote mawilii nina uzoefu wa kutosha. katika utumishi wangu serikalini mpaka kufikia kustaafu nimeona hotuba nzuri na mbaya zinavyoandikwa. 

Nimekuwa Msaidizi wa Viongozi mbalimbali na nimeshuhudia changamoto mbalimbali zinazowakabili na jinsi walivyokabiliana nazo. Kwa ufupi niseme tu- Urais ni more than a Good Speech; Urais is more than rhetorics (vibwagizo), Urais is more than a style, Urais is more than populist messages unazoweza kuwaahidi watu wakafurahishwa- Urais ni Taasisi. Taasisi hii ina mifumo,kanuni,taratibu na sheria zinazoiongoza. Rais ni Mkuu wa Serikali ambayo ina bureaucracy,chain of commands,institutions,agencies zilizopo kisheria na kikatiba; Rais ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambayo yana independent chain of command.

Lakini kubwa zaidi Rais ni Kioo cha Taifa, ni reflection ya wananchi anaowaongoza Ndani na Nje. Rais wa awamu ya Tano tunayemtafuta, anakuja kipindi ambacho nchi yetu ina FURSA ya Kupiga hatua Kubwa ya maendeleo, Lakini pia ina HATARI ya kupoteza mafanikio yote na kupoteza amani na usalama uliopo. At the centre of these two possibilities wapo wananchi,ambao ni mimi na wewe. 

Tukiongelea Fursa- maana yake kwa rasilimali tulizonazo, tukipata uongozi bora, tutaweza kuzitumia kwa faida ya wote na kila mtu akajisikia ni sehemu ya mafanikio ya nchi- watu wanataka basic things- ,elimu bora kwa ajili ya watoto wao ,huduma za afya za uhakika, maji safi na salama na jinsi ya kujipatia kipato cha halali ili waweze kumudu maisha. haya ni mambo yanayowezekana kupatikana kutokana na rasilimali tulizonazo. 

TUKIONGELEA hatari- maana yangu kubwa hapa ni lile ongezeko la tofauti ya walionacho na wasionacho,kuongezeka kwa umasikini. Binadamu wana limit ya uvumilivu, binadamu siku zote wanapenda kuwa na matumaini- yakipotea....hawashindwi kuamua kuopt for violence--- matukio tunayoyaona ya ugaidi ni zao la umasikini uliokithiri na kukosa matumaini. Nchi yetu haipo kisiwani...tusipokuwa makini,tunaweza kufika huko.....na tukifika huko maisha yatavurugika....hatutaweza kuwa na amani, upendo tunaohubiri humu ndani, hatutaweza kujuliana hali, kusaidiana,kusherehekea pamoja kama hali ya amani ipo tete. Hatuna uzoefu wa kukimbia nchi yetu kama wakimbizi- kwanza tutakimbilia wapi? Burundi? DRC? Comoro? Ni muhimu sana tujiweke kwenye context hii ili tuweze kufanya right judgment juu ya nani anatufaa kuwa Rais ajaye. 

Tuangalie haya na sio hotuba nzuri, tuwapime wagombea rekodi zao, tuone kama wanafanana na wanayoahidi; tuangalie mgombea amezungukwa na akina nani ili tujue tutakapompa nchi,washauri wake rasmi na wasio rasmi ni akina nani. Kwa kufanya hivyo, tutafanya maamuzi sahihi. 

Mimi binafsi Priority zangu kwa mgombea Urais- 
-Awe ni Mtu Safi (sio malaika); 
-Asiwe Mwoga kufanya maamuzi sahihi kwa wakati; 
-Awe ni mtu atakayehakikisha anatumia washauri/wataalam wazalendo wenye upeo mkubwa wa ndani na nje ili wamsaidie kufanya maamuzi mazuri kwa faida ya wote; 
-Asiwe mtu wa bendera kufuata upepo!
Watanzania tuamke.
Mungu ibariki Tanzania.

VIJIMAMBO IMENAKILI KUTOKA WHATSUP

3 comments:

Anonymous said...

NI KWELI KABISA AWE KAMA MKAPA AU JAKAYA AU RIDHIWANI

Anonymous said...

Duh kwani Hao wasafi Kweli?

Anonymous said...

au lowassa au tibaijuka