Mgeni Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, akitoa neno kwa ajili ya warsha hiyo kufunguliwa rasmi.
Mwezeshaji Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya vijana katika mipango ya maendeleo ya mkoa na wilaya.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya
Watu (UNFPA) Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, wameandaa warsha kwa ajili ya kuhamasisha na kuwajengea
uwezo watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu
kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha hiyo inafanyika katika vituo vya
Mwanza na Musoma. Katika kituo cha Musoma warsha inafanyika katika
ukumbi wa Afrilux Hotel tarehe 11 na 12 Juni 2015. Kituo hiki
kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na
Simiyu.
Washiriki wa warsha ni Makatibu Tawala
Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa
Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa
Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti
ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu ambao ni Makatibu
Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS),
Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini
mwezeshaji.
Afisa kutoka UNFPA anaeshughulikia
maswala ya vijana Bi. Tausi Hassan, akisisitiza jambo kwa washiriki
wa warsha kuhusu program za vijana katika shirika la UNFPA.
Washiriki wa warsha kutoka Sekretarieti
ya Mkoa na Halmashauri za mkoa wa Mara na Simiyu wakiwa katika picha
ya pamoja na wawezeshaji wa warsha hiyo.
No comments:
Post a Comment