Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakikagua mitaala ya kufundishia kwenye ofisi za walimu katika shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa ugeni huo.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) wakipitia baadhi ya kurasa za mwongo wa kufundishia kitabu cha Uraia wakati wa ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ametaka serikali za tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwezeshwa zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi.
Aliyasema hayo wakati alipozuru kijiji cha Chasimba mwishoni mwa juma akiwa na Balozi wa Hispania Luis Cuesta Civis kuona miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Hispania.
Mratibu huyo alisema kwamba mafanikio makubwa yanayoonekana katika kijiji cha Chasimba ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa wadau wa maendeleo na wanakijiji.
Alisema ushirikiano huo ni muhimu katika kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii.
Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo wangelipenda kuona serikali za mitaa zinawezeshwa zaidi ili kuweza kusaidia jamii kama inavyofanyika sasa katika kijiji cha Chasimba.
Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji kadhaa nchini vinavyofaidika na mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, ambao nao unachangiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo.
Alisema anapenda kuona kwamba maisha ya wakazi wa kijiji hicho yanabadilika na kuwa kama ya mama Kicheko ambaye ameondoka katika umaskini uliokithiri baada ya kutumia vyema mradi uliofikishwa kijijini hapo.
Alitoa wito kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kusaidia kuwezesha serikali za mitaa na mashirika yanayoapambana na umaskini nchini kuwezesha miradi ya kuondoa umaskini kufanikiwa.
Bi. Kicheko ambaye mwaka mmoja uliopita alikuwa hohehahe kwa sasa anatengeneza sabuni, ameboresha nyumba yake kwa kuiwekea bati na ana kula mlo zaidi ya mmoja sasa.
Katika ziara hiyo, Mratibu huyo alitaka kujua wananchi wa Chasimba katika miaka mitano hadi saba ijayo wanataka kuwaje na kujibiwa kwamba wanataka kuwa na hali bora zaidi ilivyo sasa na kuanzisha viwanda vidogo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga, alisema mpango huo wa miaka 10 ambao umeingia katika mwaka wa tatu umelenga kuwezesha afya, elimu na lishe na sasa wanafanya kuwajengea uwezo wa kuweka akiba na kuwekeza.
Alisema uwekaji akiba huo unawezekana kwa kutoa ajira wakati wa vipindi vigumu.
Alisema mpango huo wa kukabili umaskini uliokithiri unachangiwa pamoja na Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Uingereza, Shirika la maendeleo la Sweden na serikali ya Tanzania.
Alisema kuna kaya milioni moja zinazokula mlo mmoja ambazo zinatakiwa kubadilishwa kuwa katika hali bora.
Aidha alisema wameshakamilisha kutengeneza ramani ya umaskini baada ya kumaliza kuandikisha kaya maskini zilizopo nchini.
Diwani wa kata ya Yombo ambapo kijiji cha Chasimba aliyejitambulisha kwa jina la Idd alisema kwamba ni matraajio yao katika miaka 10 ijayo kubadilika kabisa kutokana na kijiji hicho kuwa na umeme na maji ya kutumia.
Alisema hata hivyo wanahitaji msukumo zaidi ili kuwa na viwanda vidogo.
Naye balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis alisema kwamba amefurahishwa na matokeo ya fedha ambazo nchi yake imezitoa zipatazo bilioni 1.3 za maendeleo ambazo nyingine zimepelekwa TASAF.
Kijiji cha Chasimba kina kaya 197 zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III (PSSN) ambapo tayari wamepewa ruzuku ya shilingi 43,227,190 katika mikupuo 9.
Imeelezwa kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa tangu kuanza kwa mradi wa PSSN kijijini hapo. Mafanikio hayo ni pamoja na kumekuwepo na ongezeko la wanafunzi wanaoandikishwa na kuhudhuria shule, aidha madarasa matatu yamejengwa na ofisi ya mwalimu.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (kulia) akiwapitisha kwenye baadhi ya maeneo katika mwongozo wa kitabu cha kufundishia somo la Urai walipofanya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakiendelea na ukaguzi katika mazingira ya shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakiwakaribisha wageni (hawapo pichani) waliotembelea shule yao wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) wakimsikiliza Mwanafunzi wa darasa la saba Nadhifa Harubu (katikati) wa shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga na Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akipitia daftari la Mwanafunzi wa darasa la saba Nadhifa Harubu (katikati) wa shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia awamu ya pili ya mradi wa TASAF iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo, huku Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) akifurahi jambo wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga (kushoto) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Yombo wakati wa ziara ya Balozi wa Spain na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa walipotembelea wilayani Bagamoyo kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF.
Bi. Kicheko Omary (kushoto) mkazi wa kijiji cha Chasimba kata ya Yombo anayenufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) akielezea mafanikio aliyoyapata tangu alioanza kupokea ruzuku za TASAF.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (wa pili kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) wakiangalia zao la Mihogo inayolimwa na Bi. Kicheko Omary (kushoto) mkazi wa kijiji cha Chasimba kata ya Yombo anayenufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) ambapo Mama huyo ameweza kuboresha nyumba yake kwa kununua Bati, Sementi, kuweka Umeme wa jua (Solar Power), kuvuta bomba la maji, Kilimo cha Mihogo, Nazi, Miwa na Mboga mboga wakati wa ziara ya siku moja kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Kulia ni Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga na Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge (wa pili kulia) Wengine katika picha ni wajukuu wa Bi. Omary, Grace Gemini (6) na Mariamu Gemini (10).
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na familia ya Bi. Kicheko Omary.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (katikati) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakiangalia zao la mboga ya Kisamvu walipotembelea shamba la Bi. Twajuana Mohamed (kulia) anayenufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) ambapo ameweza kufuga Kuku wa kienyeji, kujenga choo cha kisasa, Kilimo pamoja na kukunua mabati ya kuezekea nyumba yake kupitia mradi huo wakati wa ziara ya siku moja katika kijiji cha Chasimba, kata ya Yombo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Bi. Twajuana Mohamed (kushoto) akiwa ameongozana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga kukagua shamba la Bi. Mohamed ambaye amenufaika na mradi wa TASAF katika kujikwamua kiuchumi. Wa pili kulia ni Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie.
Bi. Twajuana Mohamed ambaye ananufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) akionyesha ugeni huo choo alichojenga baada ya kunufaika na mradi huo.
Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga kwenye picha ya pamoja na familia ya Bi. Twajuana Mohamed ambaye ananufaika na mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) sambamba na wajukuu zake.
No comments:
Post a Comment