ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 27, 2015

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo.

Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.

Na Dotto Mwaibale
MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.

Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.

"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.  


"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha  kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.

Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)

No comments: