Na Chalila Kibuda
IMEELEZWA kuwa asilimia 60 ya watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka mitano katika Mkoa wa Lindi wanautapiamlo Sugu ambao ni udumavu wa kimo na viungo vya ndani vya mwili kwa kukosa lishe bora.
Ukosefu umekuwa ukiwafanya watoto wa Mkoa wa Lindi kupata magonjwa ambayo yanachangiwa na kukosa kinga ambazo zinatokana na vyakula vyenye vitutubisho.
Hayo aliyasema Meneja mradi wa Jukwaa la lishe Tanzania(Panita) Joseph Mugyabuso wakati akieleza hali halisi ya utapimlo nchini wakati alipokutana na waandishi wa habari za watoto mjini Bagamoyo.
Mugyabuso anasema kuwa watoto wa kike wa miaka 15 pamoja na wanawake wa umri wa miaka 19 hadi 49 wamegundulika kuwa na upungufu wa damu kwa asilimia 55 katika mkoa wa Lindi ambapo ukosefu unatokana na kuwa na utapiamlo katika makuzi yao.
Anasema kuwa shughuli za mradi huo wa Panita ulioaanzishwa mwaka jana kwa ajili ya kuhamasisha jamii kula vyakula vyenye virutubisho ambavyo vitawafanya watoto kuondokana na utapiamlo ambao unawafanya kudumaa kiiakili na kushindwa kusema shule.
Mugyabuso anasema mikoa mingine ambayo imekuwa na viwango vya juu vya utapiamlo ni Mikoa ya Dodoma , Shinyanga pamoja na Iringa kwa asilimia 60.
Anasema changamoto kubwa iliyopo nchini ni ulaji duni katika familia, umasikini na mila na desturi ambao umechangia familia nyingi kula mlo moja kwa siku na kusababisha watoto waliochini ya miaka mitano kukua katika hali ya udumavu na kuendelea kuwa masikini kutokana na muda mwingi kutumia katika kuwapeleka watoto hospitali.
“Lishe ingepewa nafasi katika jamii kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa basi suala la utapiamlo litakuwa historia hapa nchini kwa sababu wazazi watashirikishwa katika lishe bora tangu wakati wa kujifungua wjawazito hadi mtoto anapofikia umri wa miezi sita”anasema Mugyabuso.
Anasema kuwa vyakula vingi vinavyozalishwa nchini havina virutubisho hali ambayo imefikia hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye utapimulo na upungufu wa damu kwa wanawake ammbao ndio wakuzi watoto katika familia.
Mugyabuso anasema kuwa katika hali ya utapiamlo familia haitaweza kuinuka katika uchumi kutokana na majukumu makubwa yanakuwa katika kuimarisha afya ya watoto ambao wameathirika na utapiamlo.
Anasema kuwa asilimia 40 ya vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja vinavyotokea kila mwaka hapa nchini vinasabaishwa na kushindwa kunyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ambapo baadhi ya wanawake wanakuwa na upungufu wa damu hali ambayo hawawezi kuzalisha maziwa ya kuwanyonyesha watoto waliowazaa.
“Wazazi wa watoto wanatakiwa kuwanyonyesha kwa miezi sita mfululizo bila kuwapa chakula chochote ili kupunguza vifo vya watoto wadogo waliochini ya mwaka moja vinavyotokana na lishe duni ambapo hapa nchini asilimia 40 ya vifo vya watoto wenye umri huo vinatokana na lishe duni”anasema Mugyabuso.
Anasema kati ya watoto 10 wenye umri chini ya miaka mitano hapa nchini ,wanne kati yao wamedumaa na hali hiyo inasababishwa na lishe duni wanayopata watoto hao na kuchagiwa kula vyakula vingi lakini havina virutubisho na wakati mwingine kuchangiwa na familia kuwa na umasikini kujitosheleza katika chakula kwa ajili ya watoto hao.
Mugyabuso anasema kuwa mbali na kiasi hicho cha utapiamlo na lishe duni pia viwango vya upungufu wa wekundu wa damu kwa wanawake na watoto vipo juu kwa asilimia 77,
“ Pia asilimia 50 ya wajawazito katika mkoa huo wanaupungufu wa wekundu wa damu ambao unaosababisha Utapiamlo kwa kukosa lishe bora”aliongeza.
Anasema licha ya serikali kuanisha mradi wa urutubishaji wa vyakula kwa watoto lakini bado kuna jitihada za makusudi zinahitajika katika kupunguza tatizo hilo.
Wananchi wanasemaje kuhusu hali ya lishe
Wananchi wanasema kuwa vyakula vya nchini vinatengenezwa kwa ajili ya biashara kwa kushindwa kuweka virutubisho katika kuimarisha lishe.
Mwajuma Mohamed anasema kuwa akitaka kupata chakula cha lishe lazima atengeneze mwenyewe kwa kuchanganya na kupeleka katika sehemu ya usagishaji.
Anasema kuwa ni changamoto za familia masikini ambazo haziwezi kununua vyakula vya mchanganyiko na kuchanganya ili kuweza kupta chakula chenye virutubisho.
Magdarena Joseph Mkazi wa Tabata anasema serikali iweke sera ya wanaozalisha vyakula katika mashine vifanye mchanganyiko katika kuweza kupata bidhaa za vyakula vyenye lishe kwa ajili ya watoto na watu wazima.
Anasema kuna watu wana miili mikubwa lakini lishe ni mbaya kutokaana na kula vyakula visivyokuwa na virutubisho ambavyo vinatakiwa kitaalam.
Magdarena anassema kuwa watoto wataendelea kuwa na utampiamlo kama serikali haitweka kipaombele cha kuweka sera kuwa na watu ambao watahusika na utengenezaji wa vyakula vyenye virutubisho ili kuweza kuokoa vifo vinavyotokana na utampiamlo.
Kassimu Mamboleo anasema kuwa vyakula mbavyo tunazalisha kuna uwezekano wa kutengeza vyakula vyenye virutubisho vya lishe kwa kutolewa elimu jinsi ya kuweza kufanya uchanganyaji wa vyakula hivyo kwa wataalam waliobobea katika masuala ya lishe.
Mtandao
Nchi ya Botswana imeweza kutoa elimu ya lishe ambapo kila mwananchi amekuwa sehemu ya kupiga vita utapiamlo wakati nchi hiyo ilikuwa na kiwango kikubwa cha cha utapiamlo kwa nchi za Afrika.
Malebogo Keataretse, mama wa mtoto mwenye umri wa miaka mitano, anahakikisha kuwa ananunua ‘‘chakula chenye virutubisho kama vile mbogamboga, matunda na nafaka katika duka la vyakula na vinywaji na kuandaa vyakula hivyo kwa ufanisi kabla ya kumlisha ili kuweza kupiga vita utapimlo kwa watoto.
‘Kwa ajili ya kifungua kinywa namlisha mtoto wangu uji wa shayiri na glasi moja ya juisi. Wakati wa chakula cha mchana na cha usiku anakula kile ambacho familia inacho, ambacho ni pamoja na wali pamoja na nyama ya kusaga (ijulikanayo kama seswaa). Anapenda milo yote hii na mara chache sana anapuuzia sahani, labda kama amechoka kiakili,'' anasema.
Oarabile Matongo anasema kuwa mtoto wake wa miaka minne Thato anapenda kula vitafunwa. Thato anabeba vitafungwa kwenda kwenye shule ya awali. ‘‘Sasa anapenda vitafunwa mno kiasi kwamba hawezi kula kitu kingine chochote kile. Wakati wa jioni ninapika chakula pamoja na mbogamboga lakini anapendelea kula nyama tu.''
Hali ya kijamii na kiuchumi inabainisha kitu cha kuchagua katika milo ya watoto. Watoto kutoka familia za kipato cha chini mara nyingine wanalazimika kutokula milo mingine kama vile kifungua kinywa kutokakana na kukosekana chakula cha kutosha katika nyumba.
Magdeline Khamandisi anaiambia IPS kuwa kijana wake mwenye umri wa miaka minne Kenneth anaonekana kuendelea vizuri pamoja na kwamba anakunywa uji tu mara nyingine siku nzima.
‘‘Anakula kitu, hivyo sihitaji kumnunulia kitu chochote kile cha anasa kwa ajili ya milo yake.''
No comments:
Post a Comment