ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 27, 2015

YANGA VS VILLA HAKUNA MBABE, MSUVA APAISHA PENALTI, MWASHYUYA, KASEKE WATAKATA



Mechi ya kirafiki kati ya Yanga na SC Villa ya Uganda imemalizika kwa sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amekosa penati waliyopata Yanga katika kipindi cha pili baada ya kupaisha bonge ya ‘mnazi’.

Acha hayo yote, burudani ilikuwa zaidi kwa Geofrey Mwasyuya na Deus Kaseke ambao walicheza vizuri katika mechi ya leo.
Uwezo waliouonyesha wawili hao kwa kushirikiana na Malimi Busungu, imeonyesha Yanga inaweza kuwa na kikosi bora zaidi hapo baadaye.

SC Villa walionekana wako fiti, lakini Yanga walishirikiana na kucheza kwa kuelewana zaidi.
CREDIT: SALEHJEMBE

No comments: