ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 11, 2015

Dr Slaa athibitisha kuteuliwa na UKAWA


Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wa @twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA. 
CREDIT:MILLARDAYO

1 comment:

Anicetus said...


Wilbrod Peter Slaa

Willbrod Peter Slaa alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1948 katika kijiji cha Kwermusi, wilaya ya Mbulu.

Ni katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama kinachoongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia alikua mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili kwa asilimia 27.05 ya kura zote, akiachwa na Jakaya Kikwete wa CCM aliyeongoza kwa kupata asilimia 62.83, kadiri ya matokeo rasmi ambayo hayajasadikiwa na wananchi wote.

Kabla ya kugombea urais alikuwa mbunge wa Karatu miaka 1995-2010; baada ya kugombea urais sasa si mbunge tena.


Elimu
Willbrod Slaa alisoma shule ya msingi Kwermusi iliyoko wilayani Mbulu miaka 1958-1961 na baadaye shule ya kati (middle school) ya Karatu miaka 1962-1965.

Baada ya darasa la nne Slaa alijiunga na seminari ya Dung'unyi mkoani Singida miaka 1966-1969 na kusoma sekondari. Kisha akaendelea na masomo ya juu ya sekondari katika seminari ya Itaga mkoani Tabora miaka 1970-1971 alikohitimu kidato cha sita.

Alipomaliza kidato cha sita katika seminari ya Itaga alikuwa ameshafanya maamuzi ya kuwa mtumishi wa Kanisa Katoliki. Alijiunga na seminari kuu ya Kibosho miaka 1972-1973 na kupata stashahada ya falsafa iliyompa sifa ya kuhadiliwa na seminari kuu ya Kipalapala iliyopo Tabora kati ya mwaka 1974 na 1977 na alipata fursa ya kubobea zaidi masomo ya falsafa na teolojia huku pia akisoma stashahada ya teolojia katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda.

Baada ya safari ndefu ya kuusaka utumishi Slaa alipadrishwa (alipewa upadri rasmi) mwaka 1977 na baada ya utumishi wa miaka michache alijiunga na chuo kikuu cha Kipapa cha Urbaniana nchini Italia akisomea udaktari wa sheria za Kanisa ulio maarufu kama J.C.D. (Juris Canonic Doctor) kati ya mwaka 1979 na 1981. Katika mfumo wa Kanisa Katoliki J.C.D ndiyo shahada ya juu katika masomo ya sheria za Kanisa.

Uongozi Kanisani
Slaa alianza kuwa kiongozi tangu alipokuwa mwanafunzi pale Kipalapala ambapo alichaguliwa kuwa rais wa wanafunzi; mapadri wanasema alikuwa mmoja wa viongozi wazuri sana kupata kuongoza Kipalapala.

Pia Slaa amewahi kua msaidizi wa askofu na mkurugenzi wa maendeleo katika Jimbo Katoliki la Mbulu.

Amewahi kua Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka tisa (mihula yote mitatu). TEC ndiyo chombo cha juu cha kusimamia ushirikiano ndani ya Kanisa Katoliki Tanzania.

Slaa anaelezwa kama katibu mkuu mwenye ufanisi mkubwa tangu TEC ianzishwe. Miundombinu mingi ya Kanisa Katoliki ilianzishwa na kukamilishwa kipindi ambacho Slaa alikuwa katibu wa TEC.

Katika siasa
Slaa alijitoa kwenye upadri mwaka 1991. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maaskofu kadhaa, Slaa alifanya hivo kwa kufuata taratibu za Kanisa Katoliki na aliacha mwenyewe bila kufukuzwa, kushinikizwa ama kupewa onyo.

Aliingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge mwaka 1995 akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi kupitia tiketi ya CCM na alishinda katika kura za maoni za chama hicho. Vikao vya CCM vilipokutana Dodoma vikamuengua na kumweka tena mbunge anayemaliza muda wake, Patrick Qorro. Wananchi wa Karatu wakamuomba agombee ubunge kupitia chama kingine na ndipo Slaa alipambana na wagombea wa vyama vingine kama CCM, CUF, NCCR MAGEUZI, UDP na aliwashinda wote kwa kupata asilimia 52, akifuatiwa na mgombea wa CCM aliyepata asilimia 44.

Uchaguzi uliofuata, mwaka 2000, Slaa alishiriki na kupata ushindi mkubwa zaidi. Tena kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 Slaa aligombea kwa awamu ya tatu na kupata ushindi wa asilimia 50 dhidi ya asilimia 49 za Patrick Tsere wa CCM.

Katika CHADEMA amewahi kuwa makamu mwenyekiti kabla hajachaguliwa kuwa katibu mkuu katika mwaka ambao Freeman Mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti nao wameendelea kuongoza kwa pamoja hadi hivi sasa.

https://sw.wikipedia.org/wiki/Wilbrod_Peter_Slaa