Moja ya udhaifu mkubwa unao kumba mataifa mengi hasa barani Afrika ni kutokua na mikakati ya uzuizi na endelevu dhidi ya uhalifu mtandao. Imethibitika kua Nchi nyingi zimekua zikingoja tatizo litokee ndio jitihada zinachukuliwa kutatua tatizo huku athari ikiwa imeshaonekana.
Mwaka huu baada ya Nchi ya Ghana kua miongoni mwa waathirika wa uhalifu mtandao ambapo mtandao mkuu wa serikali ya nchi hiyo inao hudumia tovuti 58 za serikali ulidukuliwa na kusababisha tovuti 11 kuingiliwa na kuathiriwa na wahalifu mtandao; waziri wa mawasiliano wanchi hiyo Dr. Edward Omane Boamah ametangaza mapambano dhidi ya uhalifu mtandao ili kulinda usalama mtandao wanchi hiyo.
Tukio hilo la udukuzi baadae CERT ya nchi hiyo yenye dhamana ya kutambua na kuzuia uhalifu mtandao kabla haujatokea pamoja na na kuhakiki usalama mtandao wan chi hiyo unaendelea kubeba sura njema ilisema wahalifu mtandao walifanikiwa kudukua tovuti hizo za serikali na kuziathiri vibaya kutokana na mapungufu ya kutokua na program zinazoendana na wakati katika tuvuti hizo.
Katika hotuba iliyosomwa na Patricia Dovi Sampson kwa niaba ya waziri wa mawasiliano wa Nchi hiyo katika jukwaa la wadau wa maswala ya usalama mitandao Julai Mosi mwaka huu 2015, iliainisha kua nchi hiyo tayari imetengeneza sera na mkakati wa taifa wa usalama mtandao (National Cyber Security Policy and Strategy (NCSPS) document) ili kupambana na uhalifu mtandao nchini humo.
Ikisisitiza Hotuba hiyo ilieleza, Nchi hiyo inatambua kua uhalifu mtandao hauna mipaka kwani wahalifu udukuzi wa tovuti za serikali ya nchi hiyo ulionekana wametokea nchini Uturuki. Hivyo ikaelezwa, Nchi hiyo itaimarisha zaidi ufanyaji kazi dhidi ya uhalifu mtandao kwa ushirikiano na mataifa mengine ili kufikia malengo.
Hotuba hiyo pia ilihimiza vyombo vya habari kuongeza jitihada za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao kwa wanachi wa Nchi hiyo kwani uelewa bado umekua mdogo sana unaosababisha uhalifu mtandao kuzidi kushika kasi nchini humo na kuathiri uchumi kutokana na makampuni ya Kifedha ya Nchi hiyo kuonekana kuathiriwa zaidi.
Aidha, Mshauri mkuu wan chi hiyo katika maswala ya usalama Mtandao Bwana. Albert Atwi-Boasiako, alieleza mafunzo ya uelewa yanayo paswa kufanywa kwa taasisi za serikali na zisizo za serikali bado ya kiwango cha chini sana kwa kiasi kikubwa hali inayo sababisha taasisi hizo kushindwa kuwa na mikakati stahiki na endelevu ya kutambua na kudhibiti uhalifu mtandao kabla haujatokea.
Hivyo mshauri huyo alitoa Wito kwa taasisi hizo kua na mipango madhubuti ya kujipatia elimu za ufahamu dhidi ya uhalifu mtandao ili kuweza kubaki salama na kupunguza uhalifu mtandao unao kua kwa kasi Duniani kote.
Katika kuhitimisha hotuba ya Waziri wa Mawasiliano Wa Nchi ya Ghana, wito ulitolewa wa kua na njia rafiki ya ukusanyaji wa taarifa na kupata Takwimu sahihi zitakazo onyesha kiwango cha uhalifu mtandao huku intelijensia ya utokeaji wa uhalifu huo ikifanyiwa kazi ipasavyo ili kuhimili vishindo vya uhalifu mtandao nchini humo.
Nini Taifa la TANZANIA linajifunza kutokana na hili?: Ikumbukwe Tanzania pia imekua ni miongoni mwa nchi zilizo ainishwa kua na tabia ya kukabiliana na uhalifu mtandao baada ya kutokea imeaminika njia za kutambua na kudhibiti uhalifu kabla haujatokea bado ni tatizo na jitihada za dhati zina hitajika.
Kwa upande wa Sera na mikakati wa maswala ya usalama mitandao bado taifa Halina kabisa hadi sasa kitu ambacho ni changangamoto kubwa katika kupambana na uhalifu huu mtandao.
Pia Uelewa na nguvu kazi watu imeendelea kua changamoto huku nguvu kazi chache zilizoko kutotumiwa vizuri na taifa. Aidha, ushirikiano kuanzia ngazi ya taifa pamoja na kuvuka mipaka bado umeendelea kua changamoto kubwa inayo paswa kutafutiwa suluhu.
Upambanaji na uhalifu mtandao lazima uwe na mikakati na kuhaki njia stahiki zilizopendekezwa na wataalam wa usalama mtandao duniani kote zinafatwa ipasavyo ili kuhakiki taifa linabaki salama kimtandao – Bado kumekua na kusua sua kwa kuwekeza katika maswala ya usalama mitandao Nchini huku Taifa kuonekana kupiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA ambapo Serikali ya Awamu ya Nne imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwekeza katika Miundo mbinu na ukuzaji wa matumizi ya TEHAMA Nchini.
Ukuaji huu wa kasi wa Miundombinu na utumiaji wa TEHAMA ikumbukwe inaambatana kabisa na ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao Nchini. Hivyo jitihada za dhati na haraka katika kukabilia na Hali tete ya hapo baadae kimttandao zina hitajika hasa Baada ya TANZANIA kuorodheshwa kua ni Nchi ya 6 Inayotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandaokatika mwaka wa 2015/2016 huku Ransomeware kwa mara ya kwanza kuonekana kuathiri taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment