Advertisements

Wednesday, July 15, 2015

Leo Mzee Kingunge kaongea na Vyombo vya Habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.


Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha
kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu
kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya
kuheshimu katiba na taratibu za chama.
Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5
kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.


Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati
ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.


Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa
maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.


Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni
zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.


Kwa mujibu wa Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na
dharau kwa wanachama wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona
hakuna lolote tunaloweza kufanya ila mimi nitasema.


Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu
iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.


Anasema Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa
yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na
Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo
yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo.


"Nawaheshimu sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika
waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995
walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6,"
alisema Kingunge.


"Tulipofika NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo,
mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa
mara ya kwanza muundo wa Chama ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka
jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 6,” aliongeza Kingunge.


"Mimi na Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile,
Wajumbe wa Kamati Kuu walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo
yao. Mwalimu na Mimi ikabidi tuingilie kati na kusaida K'Kuu,
tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na wagombea wakaanza
kujieleza," aliendelea kuongeza.


Kingunge ameendelea kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba
NEC ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.


"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi,
lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na
“KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki
yake ya msingi ndani ya Chama.


"Kuna watu wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga
mkono, sasa ningependa kusema hivi:


"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa
ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo
sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.


"Lowassa sio kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu
- kuna viongozi wa kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani,
Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote
walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.


"Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana
ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi.
Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi
ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.


"Yote haya yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond.
Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.


Kwa mujibu wa Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo
mambo ya Chama yanaenda vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa
hilo kuwa amekitumikia chama.


Kingunge anadai Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila
sehemu aliyopitia alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo
ya wananchi.


Anadai mradi wa maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini
limewezekana chini yake Lowassa akiwa waziri wa maji.


Amesema Lowassa kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa
juzi ndani ya CCM umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.


"Zipo hadithi za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni
mawazo ya watu waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo
zote pesa zote anatoa wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa
Bakheresa asingeweza!” alisema mzee Kingunge.


Mzee Kingunge alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti
wa Chama, mwingine yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa
'Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi
wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu.


"Yalitokokea Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu
chenye kuheshimika sana nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae
lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na
demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea
Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa kusikilizwa
kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema mzee
huyo.


"Chama kilichofanya maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa
kwenye Katiba. Nawaomba viongozi wetu warudi kusoma ahadi za
mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM.
Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.” alisema
mkongwe huyo ndani ya CCM.


Kwa mujibu wa mzee Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima
kiendelee. Amesema CCM imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake
ya leo hayamhusu yeye, yeye hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.


Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama
kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini
yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili
watu watoe madukufuku yao.


Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili
kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu
Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo
na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.


Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili
wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja
ili kupambana na adui.


Mzee huyo amedai Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba
na akaendelea kubaki ndani ya Chama.


Kingunge ameulizwa wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini
hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini? Amedai 'Vitu vingine havipaswi
kusema hadharani, niliona mambo yameharibika, nikakaa na Lowassa
nikamshauri awajibike kisiasa.’


Ameulizwa kama ana mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha
kutokuridhishwa na uvunjifu wa katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka
kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi kadi yangu namba 8 na
nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi nitasema.’


Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”


Asanteni

3 comments:

Anonymous said...

Uko saes mzee na mara nyingi hii Chama imekuwa ikilalamikiwa kila siku bungeni mnabisha na kuwaona wabunge wa upinzani wabaya. Wameikalia chama kea kuwaumiza wale wenye kuwajibika kama Lowassa. Viongozibsio wawajibikaji na nakihakikishia hata mpeperusha bendera John Pombe bado ana kazi ndefu akiingia hapo mahali tena baada ya wizi wa kura kama alivyodai kada wa chama NAPE. kishindo hata kwa goli ya mkono .

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe kabisa Mzee Kingunge CCM inanuka dhuluma sana. Lowassa alianza kuwindwa na vijishetani vidogo kwenye chama. Mimi siyo mwanachama wa CCM ila kwa kusema kweli ninamkubali Lowasa kuwa ni mtu makini sana katika kazi. Hata hivyo yote ni Mbele Magufuli siyo haba ni mchapa kazi mwingine na kwa kiasi fulani pia anauzika kwa wananchi. Ndani ya CCM wangeweza kufanya kosa wakaweka hapo 'Dogi" nyingine kweli mazishi yenu yangekuwa Decemba.

Unknown said...

Hii taarifa yako ulioieka hapa inatofautina kwa kiasi kikubwa na original newslet ambayo nimeisoma michuzi blog. Hi ya happa imelenga katika kuleta chuki zaidi na kuwafarakanisha watanzania.