Wabunge
watano wamepewa adhabu ya kutokuhudhuria vikao vya mkutano wa 20 wa bunge, kwa
madai ya kukiuka kanuni za bunge na kusababisha vurugu hali iliyopelekea spika
wa bunge kuahirisha bunge.
Adhabu
hiyo imetolewa na kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge ambapo
waliosimamishwa ni Mh Tundu Lissu, Mh John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekul
na Mh Felix Mkosamali ambao hawataweza kuhudhuria vikao vya bunge hili hadi
litakapovunjwa na wabunge wengine wawili Mh Peter Msigwa na Mh Rajab Mbarouck
Mohamed wamezuiliwa kuingia vikao viwili vya bunge ambapo akisoma maamuzi hayo
mjumbe wa kamati hiyo Mh Hassan Ngwilizi amesema.
Vurugu
hizo zilitokea wakati waziri wa nishati na madini Mh Simba Chawene akiwasilisha
muswada wa sheria ya petroli bungeni mjini Dodoma ambapo wabunge wa upinzani
walianza kuomba muongozo wa spika huku Mh Chawene akiendelea kusoma muswada huo
lakini baada ya muda alishindwa kuendelea baada ya kuzidiwa na kelele za
wabunge hao hali iliyosababisha spika wa bunge Mh Anne Makinda kuahirisha
bunge.
Mara baada
ya kikao cha bunge kuahirishwa nje ya ukumbi wa bunge mbunge wa Ubungo Mh John
Mnyika akazungumzia suala hilo kwa niaba ya wabunge wa kambi ya upinzani
bungeni ambapo amesema kambi ya upinzania haiko tayari kuua ndoto za watanzania
za kuondokana na umaskini kwa kutumia rasilimali zao na hapa anafafanua zaidi
sababu za wao kupinga miswada hiyo.
Waziri wa
nchi, ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama amekanusha
madai ya miswada hiyo kujadiliwa kwa siku moja na kudai kuwa ingeweza
kujadiliwa hadi pale ambapo wabunge wangefikia muafaka na kuongeza kuwa ndiyo
maana serikali iliamua isomwe mwishoni baada ya miswada mingine yote
kujadiliwa.
No comments:
Post a Comment