Viongozi wa Kata ya Iganzo pamoja na Uongozi wa Chuo cha CBE wakiwa katika meza kuu wakati wa hafla ya kukabidhiana mikataba ya kuuziana ardhi.
Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Emmanuel Mjema akiwashukuru wakazi wa Iganzo kwa kukubali kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa Chuo.
Katibu wa jumuiya ya Igomanzo, Aman Mwazumbe akieleza namna walivyokubaliana na uongozi wa Chuo na kuwakabidhi ardhi.
Chief Ndele Wilson akitoa Baraka zake kwa uongozi wa Chuo cha CBE kuhusiana na kuendelea na ujenzi.
Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela akitoa hotuba yake katika hafla ya kukabidhiana mikataba kati ya wananchi wa Iganzo na Chuo cha CBE.
Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela akimkabidhi Mkataba Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Mjema.
Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela akimkabidhi mkataba Chifu Wilson kwa niaba ya wananchi wa Iganzo.
Mkuu wa Chuo Profesa Mjema na Chifu Wilson wakipongezana baada ya kukabidhiana mikataba.
Msema chochote(MC) ambaye pia ni mwalimu wa CBE Mbeya, Mwalimu Beni akiendelea kuendesha ratiba.
Viongozi mbali mbali wakishuhudia sherehe za makabidhiano ya mikataba.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia makabidhiano ya mikataba.
Baadhi ya watumishi na walimu wa Chuo cha CBE wakifuatilia kwa makini matukio ya makabidhiano ya mikataba.
Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma na Utafiti akitoa shukrani kwa wakazi wa Iganzo.
Baadhi ya watumishi wa Chuo wakishirikiana na wacheza ngoma kutoa burudani na kuwapa zawadi.
Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani.
Mwalimu Ben akipuliza kifaa kinachotumika katika ngoma za asili.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi, viongozi wa CBE na viongozi wa Kata ya Iganzo.
WANANCHI wa Kata ya Iganzo iliyopo jijini Mbeya na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya wamekabidhiana ardhi tayari kwa ujenzi wa Chuo baada ya kukamilishana mikataba.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mikataba ya ardhi hiyo yenye ukubwa wa hekari 55 zenye thamani ya shilingi Milion 271, Mkuu wa Vyuo vya CBE, Profesa Emmanuel Mjema aliwapongeza wakazi wa Iganzo kwa ushirikiano walioutoa na kukubali kutoa ardhi.
Alisema kutokana na makabidhiano ya mikataba ya kisheria kukamilika mchakato wa ujenzi wa Chuo utaanza haraka iwezekanavyo ili wakazi wa Iganzo waliotoa ardhi waanze kupata manufaa mapema ili kuweza kuinua uchumi wao.
Alisema Chuo kitakapokamilika watumishi watapata huduma mbali mbali kutoka katika jamii inayokizunguka Chuo ambapo pia watoto watanufaika na elimu kwani wazazi hawatahangaika kuwapeleka mbali.
Kwa upande wao Chifu wa Iganzo, Ndele Wilson na Katibu wa Jumuiya ya Igomanzo, walisema hilo eneo awali walijitokeza wawekezaji ambao walitaka kulittumia kujenga Hotel lakini wakakataa kwa kuona hawatapata manufaa yoyote hivyo kukikubalia Chuo.
Naye mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, Afisa tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa, alisema mahusiano mazuri ya wananchi ndiyo yaliyopelekea wawekezaji kuwafuata na kuomba ardhi.
Mbeyela aliwasihi wakazi wa Iganzo kuanza kufikiria shughuli za kufanya ambazo kupitia Chuo wataweza kupata manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kujikita katika shughuli za uzalishaji ili Chuo kitakapokamilika waweze kuuza bidhaa zao.
Aidha alitoa wito kwa wananchi hao kuweka wazi makubaliano yaliyofikiwa kuwa ni mikataba ya kisheria ambayo itakuwa ya milele hivyo jambo hilo linapaswa kuelezwa hata kwa vizazi vijavyo ili kuepusha migogoro isiyokuwa na faida yoyote kwa baadaye.
Katibu huyo alisema pia uongozi wa CBE unapaswa kuzisaidia shule za Sekondari zitakazokuwa zinakizunguka Chuo kwa kujitolea kufundisha masomo ya sayansi jambo ambalo pia litawasaidia upatikanaji wa wanafunzi bora.
Akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma na Utafiti, Profesa Simon Msanjila, aliwashukuru wakazi wa Iganzo kwa kujitolea ardhi na kuongeza kuwa hivi sasa Chuo kimeanzisha masomo ya Digrii ya Ualimu hivyo wakati wa mafunzo ya vitendo watatumia shule za Sekondari zilizopo jirani na Chuo.
Na Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment