ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 7, 2015

Chumba cha mtoto usipime!

chumba1
Chumba maalum cha mtoto wa Diamond Platnumz.

Musa Mateja, GPL

Staa wa Bongo Fleva Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wameandaa chumba maalum cha mtoto wao wa kike ajaye na kuweka vifaa na vitu vya gharama kubwa.

TUJIUNGE ‘WHITE HOUSE’

Kwa mujibu wa mtu wa karibu na familia ya Diamond, baada ya kutenga chumba hicho maalum kwenye ‘White House’ ya rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo Madale-Tegeta jijini Dar, kilichofuata ni kukinakshi kwa vitu hivyo vya gharama vilivyonunuliwa Afrika Kusini ‘Sauzi’, Dubai na London, Uingereza.

ETI KIMEPAKWA MADINI

Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, pamoja na vitu vingine lakini chumba hicho kina kitanda spesho cha mtoto huyo ambacho kimepakwa madini (hakutaja ni madini ya aina gani).

“Wewe fikiria, kama toileti kwake ameweka vitu vya madini inashindikana nini kwa mtoto wake mtarajiwa?
chumba1w
ANATAKA AMFUNIKE KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST

“Unajua watu hawajui lakini Diamond ana shauku ya mtoto hadi anapitiliza so anataka mwanaye hata amfunike yule North (mtoto wa kike wa mastaa wakubwa wa Marekani, Kim Kardashian na Kanye West) ndiyo maana amejaza makorokoro kibao.

DAZENI KWA DAZENI

“Mbali na hivyo, kuna vitaulo, nepi, pempasi, vitambaa na vichupi vya mtoto dazeni kwa dazeni, mafuta na poda za mtoto, tishu na pini ambavyo vimejazwa kwenye vikabati maalum ambavyo haviingizi mavumbi.

“Pia chumba hicho kina midoli mizuri ya mtoto iliyopamba masofa yaliyopo ndani ya chumba hicho ambacho hakiruhusiwi mtu mwingine kuingia zaidi ya Zari na Diamond,” kilisema chanzo chetu hicho.

GHARAMA MIL. 10

Sosi wetu huyo alifunguka kuwa, ukiacha kitanda, masofa, gharama ya utengenezaji, vikokoro vyote vinagharimu zaidi ya Sh. milioni 10 za Kitanzania.

“Unajua vitu ni vingi na jamaa (Diamond) huwa ananunua kila kukicha ‘so’ sidhani kama anaweza akawa na ‘figa’ kamili ila kwa nguo na vitu vingine vidodovidogo si chini ya milioni kumi,” alisema sosi huyo kwa sharti la kutochorwa gazetini kwa kigezo kuwa si msemaji wa familia.

HUYU HAPA DANGOTE MWENYEWE

Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimsaka Diamond au Dangote au Chibu kama Zari anavyopenda kumuita kisha kumuuliza juu ya gharama za chumba hicho ambapo alifunguka:

“Wewe ujue tu kuwa ni chumba cha gharama kubwa.

KAMA SHILINGI NGAPI?

“Vitu vingi sijanunua hapa (Bongo) na sijafanya calculations (mahesabu).

WATU WANASEMA NI KUFURU, WEWE UNASEMAJE?

“Dah! Ukweli gharama ni kubwa sana iliyotumika kukiandaa chumba cha baby girl wangu, mimi siyo wa kwanza Tanzania na duniani kununua vitu kama hivyo japokuwa kuna watu watabeza na kuongea wanachotaka.

SASA MBONA MTOTO BADO NA SIKU ZIMETIMIA?

“Hiyo ni mipango ya Mungu, mashabiki wangu wamuombee Zari ajifungue salama muda wowote.”

No comments: