ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 7, 2015

ZAWADI MASHINDANO YA JIMBO LA VUNJO (MBATIA CUP 2015) HADHARANI.

Baadhi ya viongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo akiwa katika hafla fupi ya kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano ya Mbatia Cup 2015. 
Mmoja wa Waratibu wa Mashindano ya Mbatia Cup 2015 yanayofanyika katika jimbo la Vunjo,Danielson Shayo akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa washindi. 
Baadhi ya iongozi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo. 
Msaidizi wa Mbunge James Mbatia ,Hamis Hamis akizungumza katika hafa fupi ya utambulisho wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yaliyofikia hatua ya nusu fainali. 
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo . 
Kikosi cha timu ya Wazalendo ambacho kimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali. 
Kikosi cha timu ya Himo fc kilichofanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali. 
Moja ya heka heka wakati timu hizo zikitafuta nafasi ya kucheza hatua ya Nusu fainali.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Na Dixon Busagaga,Moshi.
KAMATI ya Mashindano ya Kombe la jimbo la Vunjo maarufu kama Mbatia Cup 2015 imetenga zaidi ya kiasi cha sh Mil 6 kama zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yanayoingia hatua ya nusu fainali pili leo

Zawadi zilizotengwa ni pamoja na sh Mil 2,Kombe kubwa,Medali za Dhahabu na mipira mitatu kwa mshindi wa kwanza,Sh Mil 1,Kombe la kati,Medali za fedha na Mipira miwili kwa mshindi wa Pili huku mshindi wa tatu akipata Sh 500,000,Ngao,Medali za Shaba na Mpira mmoja.

Mwenyekiti wa kamati hiyo,Danielson Shayo alisema mbali na zawadi hizo kwa washindi,kamati pia imepanga kutoa zawadi za Jezi kwa timu nane ambazo zitafanikiwa kuigia hatua ya nane bora.

“Mshindi wan ne pia tumemuandalia zawadi ya Mpira ,mbali na jezi ambazo itakuwa imepata wakati wa kufanikiwa kuingia hatua ya Nane bora,lakini pia kuna zawadi kwa Mchezaji bora,Mfungaji bora,mlinda mlango bora,timu yenye nidhamu na kocha bora”alisema Shayo.

Shayo alisema mashindano hayo yatakayotumia viwanja vitano vya Chuo cha Ualimu,Marangu,Njia Panda,Kahe Magharibi ,Himo Polisi na Ifati yamepangwa kuchezwa kwa mtindo wa mtoano .

No comments: