Rais wa DMV Bwn. Iddi Sandaly amekabidhi msaada wa computer shule ya sekondari ya Mtibwani iliyopo Kijiji cha Mtibwani Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga. Katika makabidhiano hayo Bwn. Sandaly aliongea na Walimu na wanafunzi wa sekondari hiyo na wao kumshukuru na sasa shule hiyo ndio itakua na lab ya kwanza itakayokua na computer katika Wilaya hiyo ya Mkinga.
Rais wa DMV Bwn. Iddi Sandaly (mwenye t-shirt nyekundu) akizitoa computer kwenye mabox na kumkabidhi mwalimu.
Bwn. Iddi Sandaly akifanya makabidhiano ya Computer na mwalimu
Bwn. Iddi Sandaly katika picha ya pamoja na Walimu.
Bwn. Iddi Sandaly akiongea na wanafunzi.
2 comments:
Nakumbuka Amin alipotangaza anapeleka msaada vifaa vya afya Zanzibar watu wengine walikuwa mbogo kwa nini Zanzibar tu. lakini huyu Sandaly anapeleka Tanga hamna lawama. mmmh bora niishie hapa nisije kuambiwa natukana watu
kazi nzuri lakini isije ikawa ndiyo ufagio wa uheshimiwa siku zijazo
Post a Comment