“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi? - Kinana 04/08/2015
Wadau kutokana na kauli ya Mh Kinana aliyoitoa wakati akihutubia wanaCCM waliofika Lumumba kumsindikiza Mh Dr John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya uraisi wa JMT, alimaanisha kwamba kila aliyetia nia ya uongozi CCM na hakupata fursa hiyo ni makapi. Nijuavyo makapi ni mabaki yeyote baada ya mchujo/mchakato.
Katika mchakato ule kulikuwa na watia nia 42 na baadae 38 walifanikiwa kurudisha fomu. Katika mchujo ule ni Magufuli pekee aliibuka kidedea baada ya michujo kadhaa. Kwa mantiki hiyo aliyepita kwenye chujio ni Magufuli na wengine waliobaki ndiyo MAKAPI. Kama nilivyomwelewa Mh Kinana ina maana hao MAKAPI hata wakishindana na mgombea wao sehemu yeyote ile hawatashinda.
Kwa mujibu wa Mh Kinana alimaanisha hivi:
A. Mgombea
1. John Pombe Magufuli
B: MAKAPI ( Waliobaki baada ya mchujo)Kwa kuwa hakuna mgombea yeyote aliyefukuzwa CCM baada ya mchakato wa kumtafuta mgombea uraisi kwa Chama Cha Mapinduzi kukamilika, neno MAKAPI linabaki kuwahusu wale wote waliochujwa kwenye mchakato na yeyote (makapi) akishindana na mgombea popote pale watashindwa.
Ifuatayo ndiyo listi ya MAKAPI kulingana na kauli ya Mh Kinana:
Bilal
Lowasa
Pinda
Mwakyembe
Sitta
Nyalandu
Mwigulu
Makamba
Kigwangwala
Chikawe
Ali Karume
Mwandosya
Amina Salum Ally
Asha Rose
Membe
Wassira
Makongoro
Ngeleja
Mpina
Sumaye
Muhongo
Sanoko
Mahiga
Jaji Ramadhani
Dr Mwele
Murenda
Boniface Ndembo
Bw Bilohe (Mkulima)
Peter Nyalali
Helen Elinewinga
Anthony Chalamila
Dk Muzamil Kalokola nk.
Wadau kutokana na kauli ya Mh Kinana aliyoitoa wakati akihutubia wanaCCM waliofika Lumumba kumsindikiza Mh Dr John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya uraisi wa JMT, alimaanisha kwamba kila aliyetia nia ya uongozi CCM na hakupata fursa hiyo ni makapi. Nijuavyo makapi ni mabaki yeyote baada ya mchujo/mchakato.
Katika mchakato ule kulikuwa na watia nia 42 na baadae 38 walifanikiwa kurudisha fomu. Katika mchujo ule ni Magufuli pekee aliibuka kidedea baada ya michujo kadhaa. Kwa mantiki hiyo aliyepita kwenye chujio ni Magufuli na wengine waliobaki ndiyo MAKAPI. Kama nilivyomwelewa Mh Kinana ina maana hao MAKAPI hata wakishindana na mgombea wao sehemu yeyote ile hawatashinda.
Kwa mujibu wa Mh Kinana alimaanisha hivi:
A. Mgombea
1. John Pombe Magufuli
B: MAKAPI ( Waliobaki baada ya mchujo)Kwa kuwa hakuna mgombea yeyote aliyefukuzwa CCM baada ya mchakato wa kumtafuta mgombea uraisi kwa Chama Cha Mapinduzi kukamilika, neno MAKAPI linabaki kuwahusu wale wote waliochujwa kwenye mchakato na yeyote (makapi) akishindana na mgombea popote pale watashindwa.
Ifuatayo ndiyo listi ya MAKAPI kulingana na kauli ya Mh Kinana:
Bilal
Lowasa
Pinda
Mwakyembe
Sitta
Nyalandu
Mwigulu
Makamba
Kigwangwala
Chikawe
Ali Karume
Mwandosya
Amina Salum Ally
Asha Rose
Membe
Wassira
Makongoro
Ngeleja
Mpina
Sumaye
Muhongo
Sanoko
Mahiga
Jaji Ramadhani
Dr Mwele
Murenda
Boniface Ndembo
Bw Bilohe (Mkulima)
Peter Nyalali
Helen Elinewinga
Anthony Chalamila
Dk Muzamil Kalokola nk.
8 comments:
Ndio makapi lakini kiswahili kinaraha yake au wewe mtoa mada hapo juu umeamua kujipotosha kwamakusudi au unaamua kuwapotosha watu nini kinana kakusudia alilopokuwa anazungumzia makapi. Kama unataka yukupepekeke kwenye darasani la kiswahili basi walimu wapo hapa, free kiswahili class. Kinana kasema nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi. Sasa suala langu kwa ndugu mtoa mada je katika majina yote ya watu ulioyataja watagombea uraisi katika uchaguzi unaokuja au la ? au lowasa na magufuli tu ndio watakaogombea katika orodha yako? Kama majina ulioyainisha watakuwemo kenye uchaguzi ujao basi kweli kama alivyosema kinana makapi yatashindana na mgombea mteule lakini kama hayo makapi ulioyataja hayatakuwepo kwenye uchaguzi sasa makapi gani unayoyanguzia kwamba kinana kawaita watu wote makapi? Katika ufahamu wangu makapi unayoyazunguzia ni mgombea mmoja aliekuwemo katika huo mchujo ambae anatarajiwa kuwepo kwenye uchaguzi na kwa maana hiyo yeye ni makapi halisi anayoyazungumzia mueshimiwa kinana. Lowasa ni makapi halisi ya CCM anayoyazungumzia kinana kwamba yatufulia yatakapokutana na mali safi kwa sababu itakuwa rahisi kwa wananchi kuyapambanua.
Wewe hapo juu mbona umerudia yaliondikwa na mwandishi au wewe ndio kiswahili hujui?wote ni makapi pamoja na lowasa jamaa ametaja list ya makapi,cha kuchekesha kuwaita ata wenzie chama cha majizi makapi .
MAKAPI NI CCM, NDO MAANA LILILOKUWA LINASTAHILI KUCHUJIKA WAKAMWOGOPA MAPEMAAAAAAA. KIDUMU CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.
KIFE CHAMA CHA CHUKUA MAPEMA
ni kweli kabisa wote ni makapi, pia hayo hayo makapi yaliyobaki ndani ya ccm yapo ambayo yamepewa dhamana ya kugombea nafasi nyingine za uongozi, swali hivi hakukuwepo watu wengine wa kupewa dhaman hiyo badala ya hayo makapi? mimi nadhani ni maneno tu ya wanasiasa ili kuwaharibia wengine. pia ukiona kiongozi anatoa maneno kama hayo ujue kabisa kaishiwa kimawazo kama walivyoishiwa hawa jamaa wanaotoa hayo maneno. ushauri wangu nawaomba watafute hoja za msingi pia kama watapata tena nafasi ya kuiongoza hii nchi basi wawe makini katika kutekeleza na kusimamia maendeleo. pia sina hakika na hilo kama wanaliweza maana wameshindwa kipindi cha miaka 50 je wataweza ndani ya miaka 5?
Ni makapi kwa sababu Kinana kasema? Au kwa sababu CCM hawakuwachagua? CCM huwa inajua kuchagua nini zaidi ya kofia na kanga?
Meno ya Tembo yake yaliyonaswa Zurich
Ache kusema ya wenzake nasi tutaeleza
Mahala pa uzalishaji, kampuni au shirika hupokea malighafi inayotumia kuzalisha bidhaa inayotakiwa na wananchi. Wakati malighafi inatengenezwa kuna sehemu ya malighafi ambayo inaoenekana kwa wakati huo kuwa siyo sahihi kwa kutengenezea bidhaa husika hivyo huchujwa na kuwekwa sehemu pembeni kwa ajili ya kuboreshwa na au kuwa recyled na kuwa malighafi ya kutengenezea bidhaa aina nyingine au yenyewe kutumika kwa shughuli zingine. Wakati huu wote huu hiyo malghafi mpya bado ni ya maana na ya maufaa shirika. Lakini kuna sehemu nyingine ya hiyo malighafi iliyochujwa wakati bidhaa zinatengenezwa inakuwa haiwezi kutumika tena kwa ajili umuhimi wake unakuwa umekwisha na hauwezi hata kuboreshwa. Hii ndio sehem katika uzalishaji inayoitwa makapi. Hata ukifanya nini makapi haya hayatasaidia chochote na hivyo ni ya kutupa tu na mengine yanaishia kuzikwa ardhini kama yanahisiwa kuwa yanaweza kuwa na madhara kwa binadamu, wanyama, mimea na vinginevyo. Hivyo Kinana alivyoongea juu ya makapi alikuwa haongei juu ya malighafi ambayo imebaki kiwandani kuendelea kuwa na manufaa katika shughuli za uzalishaji. Kinana alikuwa anaita makapi yale ambayo hayana maana tena kiuzalishaji na hivyo yametupwa kwa njia moja au nyingine kwani kuna makapi mengine hayangojei kutolewa na mtu bali yanajitoa yenyewe kwa njia zake. Kwa mantiki hii orodha ya majina ya waliotajwa na mwandishi hapo juu siyo orodha ya makapi kwani wote hao bado wako kwenye chama chao na wanendelea na shughuli za chama kama kawaida. Makapi ni hao ambao wametoka na wale ambao watatoka kwenye chama hicho wakifikiria kuwa wakienda chama kingine watakuwa malighafi huko. Ukweli tu ni kuwa uhamiaji wao huo unalengo la kwenda kusabbisha vuruga tu kwenye vyama vyao hivyo vipya kama tunavyoshudia hivi sasa. Hawa watu kweli wangekuwa na nia ya kuihama CCM kwa ajili ya kuleta mageuzi wangekuwa wamefanya hivyo zamani badala ya kusubili kuenguliwa eti ndio wanaona CCM ni mbaya. Na kwa nini wanasubili wakati huu muhimu na mfupi uliobakia kuelekea kwenye uchaguzi! Hawa watu wanataka tu kuwa changanya akili raia wema na wanachama bora wa vyama vya upinzani na hivyo kuwafanya wagongane na viongozi wao shupavu na ambao wamelewana kwa muda mrefu.
Kwa wale wanao ijua biblia... jiwe walilolikataa wahashi...nalo ni jiwe la pembeni. Leo hii karibu dunia nzima inahubiri habari za. Yesu,hata hao walio mkataa. ...hivyo ccm wamemkataa Lowasa, lakini usishangae wao ndo watakuwa watu wa kwanza kwenda kumuomba msamaha.
Post a Comment