Thursday, August 20, 2015

Matukio mbalimbali yaendelea kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwa pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakichanganya saruji, kokoto na mchanga ili kupata zege kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi ikiwa ni uzinduzi wa kuanza kwa ujenzi wa vyoo 22 kwenye Shule ya Msingi Kiboriloni, Mkoani Kilimanjaro. Uzinduzi huo ni tukio mojawapo kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa Ujenzi huo umedhaminiwa na UNDP. 
Bw. Alvaro akiweka jiwe la msingi kuzindua kuanza kwa ujenzi wa Vyoo hivyo 
Balozi Mushy naye akiweka tofali katika msingi huo 
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem naye akimpatia fundi tofali la ujenzi wa vyoo hive 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza mbele) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez,kwa pamoja wakimimina zege kwenye msingi wa Vyoo vinavyojengwa katika Shule ya Msingi ya Kiboriloni 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza katika uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vinavyojengwa katika shule ya msingi ya Kiboriloni 
Juu na Chini ni Balozi Mushy akizungumza na wanafunzi wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 katika Shule hiyo 
Wanafunzi wa Shule hiyo wakionekana kuwa na furaha na matumaini baada ya uzinduzi wa Vyoo hivyo vya Shule yao. 
Sehemu ya Uongozi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni 
Wananchini na waalimu wa shule hiyo wakisikiliza kwa makini 
Dkt. Kanem akizungumza kwenye uzinduzi wa Ujenzi wa vyoo 22 vya shule ya Msingi Kiboriloni 
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem (kulia) akifurahia jambo na Balozi Mushy (katikati), pamoja na Bw. Alvarp 
Balozi Mushy akimtambulisha Bwa. Alvaro kwa waalimu wa shule ya msingi ya kiboriloni waliojipang kumpokea 
Balozi Celestine Mushy akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Alvaro 
Bwa. Alvaro (wa nne kutoka kulia) na Balozi Celestine Mushy wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi na waalimu wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kiboriloni 

Picha na Reginald Philip

1 comment:

Anonymous said...

UNDP mana yake ni maendeleo ila leo hata wanatujengea vyoo yaani tunajenga shule vyoo hatuwezi. Mbona wasijenge shule tukajenga vyoo wenyewe?