Advertisements

Friday, May 31, 2013

Tanzanian Ladies Night - June 1st 2013.

***** Tickets Zimekwisha ***********

Tunapenda kuwaarifu kuwa ticket za shughuli hii zimekwisha kwa hiyo hatutauza ticket mlangoni.

- Tunapenda kuwashukuru wakina mama wa kiTanzania (na wakina baba ) kwa support yenu.

- Vilevile tunapenda kuwaarifu kuwa shughuli ya Tanzanian ladies Night itaanza saa 2:30 usiku (8:30PM), ila unaweza kufika saa 2:00 usiku (8:00 PM) ili upate parking nzuri vilevile ujipatie picha kwenye red carpet. Address ni 1600 New York Ave NE, Washington, DC 20002

- Tafadhali zingatia muda kwa sababu muda wa chakula ukiisha, vyombo vyote vitaondolewa.

Kwa wale mtakaofika mapema kutoka out of town, tafadhali tembelea mgahawa wa kiTanzania unaomilikiwa na mTanzania wa Kilimanjaro Passion kwa Meet, Greet and Mingle kwa siku ya Ijumaa na Jumapili. Address yake ni 2310 PRICE AVENUE, WHEATON MD 20902 namba ya simu ni 301-661-6207


Ahsanteni, TANO ladies.

31 comments:

Anonymous said...

Big up Sisters..mamabo mazuri yanaanza na wakina mama nakubali, I can't picture my self hapa nilipo leo bila ya mama yangu mzazi. HONGERENI sana.

Anonymous said...

Safi sana wadada. Mna mawazo na mitazamo chanya. Nawaomba muwe chachu ya kuhimiza wadada wenzenu wa kitanzania hapa unyamwezini kujiendeleza kielimu kama ninyi. Tunafahamu kama schedule zimebana lakini wadada mkitenga muda wa kujiendeleza kielimu kama hawa watano, mtajikuta mnatumia muda mfupi ku-earn good income kuliko kinyume chake hivi sasa. Mwanamke akiendelea, familia nzima imeendelea. Wanawake oyeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Naomba watoa maoni mnaonifuatia msinishambulie jamani, hakuna nilichokosea.

baraka daudi said...

Tano Ladies hongera sana,ideas nzuri.

Anonymous said...

mmhh....

Anonymous said...

HI FIVE TANO Ladies!!!!!!mie nishanunua tiketi yangu na subiri Juni mosi nije kushehereka.Mwenyezi mungu awaongoze na kuwalinda.
nawapendajeee...salam kutoka Kansas.

Mwanaidi Maajar said...

HONGERENI SANA TANO LADIES. Nawafahmu nyote na nina imani kubwa MTAWEZA! Nawakumbuka sana. Nawapenda. Da Mwanaidi

TANO Ladies said...

ASANTENI SANA SANA!!!

Anonymous said...


I have to ask this question. Jee kukutana is the only goal? How about majority of Tanzania woman here in USA who are struggle through paycheck to paycheck.

I hope this is not another cash flow model for 5 ladies.

Mdau

Anonymous said...

Yeahhh mmmhhhh....??????!!!!!!!!!!'.......

Projestus said...

Kwanza nawapongeza.
Mimi ni mfurukutwa wa maendeleo ya watanzania kiujumla waishio America na siyo wanawake tu!na wote wenye kutaka kuleta mabadiliko ya watanzania kiujumla.
Shida ninayo ipata kuhusu vikundi vilivyoanzishwa hapa America wengi wanafikiria kuhusu kukutana kula na kunywa tu.Nawaombeni TANO LADIES onyesheni utofauti wenu na vikundi kede kede vikiwemo vya makanisa ya watanzania kuhusu kuwaza maendeleo kwa upana zaidi na siyo kula na kunywa.Najuwa mnahitaji sana mchango wa wataalamu mbali mbali mfano:(hata kuwa mbele ya kamera bado unahitaji kuwa na mazoezi)Mkiitaji mchango wangu niko tayari.

Anonymous said...

Hayo yao, nawe saidia wa pay check to paycheck.

Anonymous said...


Ya mzee Proje! ni kaliiii!
Haya Tano ladies mshapata mtaalam volunteer! Hongera.

Anonymous said...

Nishanunua tiketi,tusubiri siku. Maendeleo huletwa na wanaethubutu,ninyi mmeweza,asanteni sana. Ombi,kuwe na dialogue za kuleta changamoto za goal,strategies,implementation and structure of how to achieve the goals. Sio kudansi na kunywa,fashion show,etc....,next time hamnioni. Mdau# 2,toa sifa sio dharau ooh! Shule,i wonder how far u r educated urself? Comment kama hizi hazina tija. Wengine hawako interested na vitu kama hivyo. I bet wewe ni mwanaume usije kuvalishwa sketi tu. Dj Luke usibanie hii pse.

Anonymous said...

sina nguo kitenge na ninatamani sana kuja,siruhusiwi kuja?

Anonymous said...

Samahani hii hella.yote kukutana tuu

bagasa said...

Tano leadies,

Safi! Nimependa hii statement " empowered and informed". Very good with this. Information is power. Kwa maana nyingine "False knowledge is more dangerous than ignorance."

Overall, great idea-just sustain it.

Anonymous said...

Nimefurahishwa sana na ninyi TANO LADIES mie ni mdau niishio Sacramento siwezi kuhudhuria kutokana na personal issues ila nawaomba sana sana sana, muwe kikindi cha tafauti yaani muonyeshe changamoto na umuhimu wa kuwa mwanamke sio DMV tu bali popote America wewe kama mwanamke wa ki-TZ. BIG UP LADIES.

Anonymous said...

Naomba tu nikujibu wewe mdau uliye uliza wakina mama wanao ishi from paycheck to paycheck watasaidika vipi? Mie naona uende tu kwenye mkutano waweza kutana na mama mwenye kuhitaji house girl/house help au baby sitter uka tengeneza pesa ya ziada kuongezea hiyo paycheck yako. UKIMWEZESHA MWANAMKE MMOJA UMEIWEZESHA JAMII NZIMA. GET INSPIRED! GET INFORMED AND GET GOING.....HEHEHE

Anonymous said...

Jamani kwanza hongereni 5ladies na hiyo motto yenu Mwanamke hupo wapi?imenigusa mtu Kama huwezi lipa $65 si lazima majungu ya nini hiyo ndiyo unaambiwa mdomo haulipiwi tax na majungu ya pembeni hayavahi Kama kweli msemaji jitokeze wape nguvu siyo kashifa

Baraka Daudi said...

Tano Ladies,mambo yameshaiva. Vizuri sana nawaombea hii shughuli iwe ya mafanikio makubwa na kuweza kumsaidia na kuonyesha jinsi kina mama wa Kitanzania wanaweza kufanya mabo makubwa. Kina baba tupo mstari wa mbele kusukuma gurudumu hilo. BIG UP SISTERS.

Anonymous said...

Haya Wanaume tumepigwa 'stop' tusije, na sisi ndio waamuliaji ngumi zikitokea, Haya mkipigana shauri yenu..set

Anonymous said...

We Anonymous wa 1.18 PM unawzia ngumu wenzako wanawaza maendeleo ndio maana wanaitwa. Tano Ladies wana maana yao wanayoijua wao watashare siku wakikutana na wlwanawake wezao watakao kuwepo siku hiyo. Kina Java pumzikeni.

Anonymous said...

Mie nipo nje ya USA nawashauri Tano ladies mkitaka maendeleo na kuheshimiwa msi side na upande mmoja wa watu, kumbukeni wa TZ tunstoka katika maisha tofauti nchini kwetu.

hivyo wachukulieni watu kama binadau, na sio kuona kikundi hiki na kile na class achaneni na watu watakaotaka muwe na wengine na musiwe na wengine.

nasema hivi sabau nimeona kwa mitandao huko marekani kuna vikundi sanana watu hawajichanganyi vileeeee hii ni kutokana na picha nazoona online na kusikia.

Mkiweka watu wote sawa bila kusikiliza hawa na kuacha kusikiliza kule, mtaheshimika na kujijenga sana.

Wasaidieni watu bila majungu au kuongea story zao nje, yaani mtu akija kwa ushauri au anatafuta kazi au chochote wekeni siri zao na mtabarikiwa sana. Msitangaze ya watu kuwacheka as na nyie hamjui kwesho.

pia msisikilize watu na majungu, as wakiona mpo pamoja lazima wataanza au wameshaanza kuwasema sema ili mgombane, salini na muwaambie kama una lakusema please nawaita wenzangu na sema mbele zao...hii ni watataka mgombane tu na mwaka kesho tutasikia hampo pamoja.

Umoja ni nguvu wa mamii wenzangu,nawatakieni kila la kheri, ila kwa wengine kufuata mfano wenu mngesema kwa kirefu hata kwenye vi intro vya facebook plae about hii/lile nyie lengo lenu ni nini na nini.

maana najua mmejiunga ila nimewasoma sana ila bado sijajua lengo lenu kubwa la kuwa pamoja, na kuweka hii event. ni vizuri mngarusha agenda etc na itavutia sana watu wengin kuja hata wale wasio karibu nanyi.

msifuate makundi au kudharau wengine, wasalimieni, wachekeeni kokote mtakapoonana nao ndio mwenda ladies

Wishing you all the best

Caroline

Anonymous said...

Kaka hapo juu asante kwa offer lakini maamuzi ya kuhakikisha usalama yameishafanywa walinzi wa usalama wakatuwepo kwenye ukumbi na atakayevuruga amani na kutuharibia shughuli yetu HATUTOMVUMILIA, kwani tuna wageni toka nje ya nchi na nje ya DMV hatutosita kumchukulia hatua za kisheria, tupo katika nchi ya sheria na wote tunazijua so ladies karibuni tufurahi pamoja. Tunawahakikishia kuwa you will all be safe!

TANO LADIES.

TANO Ladies/facebook said...

ASANTE DA CAROLINE TUMEKUELEWA NA TUTAFANYIA KAZI MAONI YAKO.

Anonymous said...

wewe mwanaume hapo juu nyinyi ndo mnatakiwa kufunza wanawake zenu wanaogombana kwenye mashughuli na kuharibu shughuli za watu,Tafadhali sana TANO Ladies hatuhitaji MABODIA kwenye shughuli ya Tanzanian Ladies Night.WANAWAKE TUPO.HALOOOOOOO

Anonymous said...

sijapenda eti wanawake mko wapi???imekekaa kimbea zaidi unafki.com mmh nextime ....

Anonymous said...

Mimi nimewaelewa "wanawake mko wapi?" maana hamsikiki huko Marekani zaidi ya vituko kwenye facebook and blogs. Its time up kuanza kufanya mambo ya maana tuyaone. Lets go TANO LADIES TUMEWAPATA!

Anonymous said...

Wewe usiyeelewa huu msemo "wanawake mko wapi?" ngoja nikusaidie, tupo wanawake wengi sana wa kitanzania hapa Marekani na wenye profession tofauti, tuna wahadhiri katika vyuo mbalimbali,waalimu wa shule, manurse, madaktari, wanasheria, wanasayansi,accountants, wajasirimali, wachumi, madiplomats the list goes on and on swali ni kuwa baada ya kuishi ughaibuni kupata elimu na exposure ya dunia ya kwanza tunaitumuiaje kujiemdeleza wenyewe hapa Marekani na kusaidia kujenga nchi yetu. Nchi hujengwa na watu na watu wenyewe ni sisi. Ndo maana tunaona Jewes communities nchi yeyote ile ukienda utaona wanaanzisha shule zao, day care zao na wanafanya vitu vingi kama jumuiya hawasubiri serikali wala chama kuwaendeleza wanajiendeleza weyewe. Swali wanawake wa Marekani tupo wapi?? Mbona hatusikiki kwa chochote cha maendeleo. Nadhani that is the meaning na SI UMBEA!!!!!!!!!

Anonymous said...

hiyo ni motto yao ndiyo maana unakimbilia unafiki,hapo nimekupata hapo juu maana hawasikiki na next time watatoa nyingine kaza boot Tano ladies

Anonymous said...

Mkichemsha sasa heheeeeeee nitachekaje mieeeee.