Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Vwawa wakiwa wambeba juu Fanuel Mkisi mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza, kura za Maoni kumpata mgombea Ubunge uliofanyijka jana katika kanisa la Moravian Mjini Vwawa. (Picha na Kenneth Ngelesi)
Mshindi wa nafasi ya kwanza uchaguzi wa marudio kura za maoni wa kumpata mgombea atakaye peperusha bendera ya chma cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) Jimbo la Vwawa Fanuel Mkisi akiwa juu ya gari huku akipunga Mikono kwa wafuasi wa chama hicho jana mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza kwa kupata kura 111.
Na Kenneth Ngelesi, Mbozi
KADA wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Funuel Mkisi ameibuka kidedea kwa mara nyingine katika marudio ya kura za maoni za kumpata mgobea atakaye peperusha bendera ya chama hicho nafasi ya Ubunge jimbo jipya la Vwawa.
Akitangaza matokeo hayo katika Kanisa la Moraviana Mjini Vwawa msimamizi wa Uchuguzi Joseph Fyume kutoka Songea alisema kuwa Mkisi ameibuka kidedea baada ya kujikusanyia kura 111 kati ya kura 179 zilizopigwa.
Alisema kuwa wapiag kura walikuwa 179 ambapo hakuna kura iliyo haribika na na kwamba zoezi hilo limeenda vizuri licha ya kuwepo misuguano ya hapa na pale ambayo wajimbe walikuwa wakionysha kutoamiana kwa kiasi fulani.
Uchaguzi huo ulishirikisha makada 13 wa chama hicho ambapo nafasi ya pili ni Abaram Msyete aliye ambulia kura 28 wakati nafasi tatu alienda kwa Steven Mwamengo kura 19 wakati kura zingine wakigawana.
Wagombea wengine ni Solomon Kibona,Babu Mwapashi,Gifrt Kalinga,Fadhili Shombe,Gerald Silyumba,Nzenga Simbeye Furaha Mwazembe,Andrew Bukuku,Dickson Kibona na Jonadhan Mwashilindi ambapo kati ya hao wangine waliambulia sufuri.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi Mkisi alisema kuwa aanshukuru wajumbe kuonysha imani kwake kwa mara nyingine kwani licha ya uchaguzi wa awali kutoridhiwa na baadhi ya wagombea lakini bado ameshinda nafasi hiyo kwa kishindo.
Alisema kuwa amekuwa akifanya saiasa kwa muda mrefu anaamani kuwa anauwezo ya kunyakua jimbo hilo kwa kushikirikiana na wanachadema wote huku akiwapongeza kamati kuu taifa kukubali uchaguzi huo urudiwe kwani umekata mzizi wa fitina na kuondoa manung’uniko ambaye yangeweza kujitokeza.
Katika uchaguzi wa awali ambao ulifanyika Julai 21 mwaka huu ambapo Msyete alijiondoka katikati ya mchakato kutokana na kutoridhishwa za hali ilivyo kuwa siku hiyo na kulamika kukata rufaa,Mkisi aliongoza kwa kupata kura 136 akifatiwa Mwamengo kura 42 na nafasi ya tatu alikuwa Jonadhani Kinona ambaye aliambulia kura 22 tu.
No comments:
Post a Comment