ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 5, 2015

SPIKA MAKINDA AZINDUA MAONESHO YA NANENANE MBEYA‏

 Spika wa Bunge, Anne Makinda akizungumza na wakulima pamoja na maafisa mbali mbali katika uzinduzi wa maonesho ya nane nane Kanda Mbeya.
 .Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonesho ya nanenane.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa akitoa utambulisho kwa wageni mbali mbali.
 Makamu Mwenyekiti wa TASO Kanda, Crispin Mtono akitoa taarifa ya maandalizi ya nanenane ya mwaka 2015 katika sherehe za uzinduzi wa maoneshihayo.
 Wageni mbali mbali wakiwa jukwaa kuu.
  Wakuu wa idara za serikali na mashirika binafsi wakiwa pamoja na wakulima na waoneshaji wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa maonesho ya nanenane.
Vikundi vya burudani vikitoa burudani kwa wageni mbali mbali.

WAKULIMA na Wafugaji nchini wametakiwa kutumia taarifa kutoka vituo vya utafiti ili kuendeleza na kuboresha mbinu bora katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Wito huo ulitolewa  na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Anna Makinda alipokuwa akizindua maonesho ya 13 ya nanenane yanayofanyika kikanda ya Nyanda za juu kusini kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Spika Makinda alisema Mikoa ya Nyanda za juu kusini inaongoza na kusifika kwa uzalishaji wa mazao ya Chakula nchini lakini kiwango bado ni kidogo hali inayosababishwa na kutotumiwa vizuri kwa taarifa za watatifi wa kilimo na mifugo.

Alisema hivi sasa hali ya uzalishaji wa mahindi ni Tani 3 kwa Hekta moja lakini watafiti wanasema Hekta moja inapaswa kutoa Tani saba za mahindi, Maziwa Ng’ombe mmoja hutoa lita 8 hadi 12 kwa siku kwa sasa na taarifa za kiutafiti zinaonesha ni Lita 24 hadi 40 jambo linaloonesha uzalishaji bado uko chini ukilinganisha na sifa ya mikoa husika.

Aliongeza kuwa maonesho ya nane  ni sehemu ya kujifunza mbinu mbali mbali za kilimo na mifugo pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa hivyo ni jukumu la viongozi mbali mbali kufuatilia baada ya maonesho kama wakulima wanayafanyia kazi mafunzo waliyoyapata kipindi cha maonesho.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi maonesho hayo, Kaimu Mwenyekiti wa Sekretariet ya  Kanda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, mbali na kumpongeza Spika kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni rasmi alisema uwanja wa nane nane unakabiliwa na changamoto chache ambazo wanauwezo wa kuzikabili.

Alizitaja Changamoto hizo kuwa ni pamoja na utafutaji wa fedha za kujenza barabara za lami kuzunguka eneo la uwanja ili kupunguza vumbi jambo ambalo litatekelezwa kwa kila Halmashauri kuhakikisha wanachangia fedha za mradi huo.

Aliongeza kuwa Changamoto nyingine ni upatikanaji wa masoko ya mazao yanayozalishwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini jambo ambalo alisema utekelezaji wake ni pamoja na kushirikiana na Nchi za Sadc ili kupata soko la pamoja suala litakalotekelezwa mwaka 2016.

Mwambungu alisema suala lingine ni mahusiano tofauti kati ya vitu vilivyo kwenye mabanda na hali halisi ya mambo yanayofsanyika mashambani mwao hali inayosababisha Wakulima na waoneshaji kushindwa kuleta bidhaa zinazoleta ushindani.

Naye Makamu Mwenyekiti wa TASO Kanda ya Nyanda za juu kusini, Crispin Mtono alisema katika maonesho hayo kuna washiriki jumla ya 466 kutoka sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, ushirika na wadau wengine kutoka sekta binafs.

NA MBEYA YETU

No comments: