Profesa Nguyulu Ibrahim Haruna Lipumba (CUF) - Makamu
Freeman Aikaeli Mbowe (Chadema) - Mambo ya Nje
Halima James Mdee (Chadema) - Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
John John Mnyika (Chadema) - Fedha na Uchumi
David Kafulila (NCCR-Mageuzi) - Kazi na Ajira
David Ernest Silinde (Chadema) - Tamisemi
Dk. Emmanuel John Makaidi (NLD) - Viwanda, Biashara na Masoko
James Mbatia (NCCR-Mageuzi) - Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Joseph Selasini (Chadema) - Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Magdalena Hamisi Sakaya (CUF) - Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Masoud Abdallah Salim (CUF) - Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)
Mchungaji Peter Simon Msigwa (Chadema) - Maliasili na Utalii
Mhandisi Mohammed Habib Juma Mnyaa (CUF) - Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
Pauline Phillipo Gekul (Chadema) - Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi (Chadema) - Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma)
Rajab Mohammed Mbarouk (CUF) - Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Tundu Antipas Lissu (Chadema) - Sheria na Katiba
Wilfred Muganyizi Lwakatare (Chadema) - Ofisi ya Rais (Utawala Bora)
Na Daniel Mbega
UKAWA wameokota almasi kwenye mchanga wa pwani, na kwa kumpata Edward Lowassa Umoja huo wa Katiba ya Wananchi unaamini utachukua dola ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Lowassa, waziri mkuu aliyelazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya kinyonyaji ya kampuni za ufuaji umeme wa dharura za Richmond na Dowans, ameshawishika kujiunga na umoja huo kupitia Chadema, hali ambayo wachambuzi wengi wa masuala ya siasa wanasena kuna kila dalili za kuung’oa utawala msonge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho huenda baada ya Oktoba itabidi kiunde Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB).Duru za siasa kutoka ndani ya Ukawa zinaeleza kwamba, ilikuwa kazi ngumu kumshawishi Lowassa kuhamia Ukawa baada ya kuenguliwa na CCM katika kinyang’anyiro cha urais, lakini kwa sasa kazi itakuwa rahisi zaidi kushinda uchaguzi wa mwaka huu kutokana na mwanasiasa huyo kuwa na wafuasi wengi nyuma yake.
Mchakato unaoendelea hivi sasa, kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, ni kuangalia nani kati ya viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo atashika nafasi gani, ingawa tayari maafikiano yanakaribia kufikia tamati.
Taarifa zinasema kwamba, ikiwa Lowassa atagombea urais kupitia Ukawa akitokea Chadema, basi mgombea mwenza – ambaye ndiye atakayekuwa Makamu wa Rais – atakuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), mchumi Profesa Nguyulu Ibrahim Haruna Lipumba.
Habari za ndani zinaeleza kwamba chini ya makubaliano ya Ukawa ikiwa mgombea urais atatoka Chadema, mgombea mwenza akitoka chama kingine itabidi ahame chama chake ili aingie chama alicho mgombea urais ili kukidhi matakwa ya kikatiba.
“Tutakaposhinda uchaguzi, kama makamu wa rais atatoka CUF itabidi kila akitoka katika ofisi ya makamu wa rais, kituo cha kwanza atasimama Makao Makuu ya CUF kwa ajili ya kupeleka taarifa na kupata baraka za chama katika masuala muhimu,” chanzo kimoja kilinukuliwa kikisema.
“Kazi imekwisha, hivi sasa watu wanapanga mikakati ya nani awe nani baada ya uchaguzi, najua Lipumba atakuwa makamu wa rais na hiyo inaweza kuimarisha serikali kwa sababu Lowassa ni mchapakazi asiyependa masikhara na makamu wake ni mchumi aliyebobea,” alisema mmoja wa watu walio karibu na viongozi hao.
Hata hivyo, katika upangaji wa uongozi, inabainishwa kwamba Dk. Wilbrod Peter Slaa ndiye aliyepangwa kuwa Waziri Mkuu na kujenga safu imara ya uongozi wa juu wa taifa, lakini kitendo chake cha kukaa pembeni hivi sasa kimeweka doa kambi hiyo ya Ukawa.
Vyanzo hivyo vinawataja wabunge kadhaa wa vyama hivyo waliomaliza muda wao kwamba ndio wanaopigiwa chapuo kuongoza wizara mbalimbali, japokuwa wapo baadhi yao ambao wameanguka katika kura za maoni.
“Mhandisi Mohammed Habib Juma Mnyaa ameshindwa kwenye jimbo lake la Mkoani huko Pemba, lakini huyu jamaa ndiye anayefaa kuongoza Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambayo aliiongoza akiwa waziri kivuli.
“Yupo pia Mhandisi aliyebobea, Dk. Emmanuel John Makaidi, ambaye anastahili kuongoza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa ufanisi mkubwa,” mjumbe mmoja kutoka CUF.
Taarifa hizo zinasema, Dk. Makaidi, Mwenyekiti wa chama cha NLD kinachounda Ukawa ambaye alipata kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba kabla ya kurithiwa na Juma Salum, anaweza kuteuliwa na rais kutoka kwenye ‘kapu’ badala ya kuingia majimboni kupigana vikumbo, fursa ambayo pia anaweza kuipata Mhandisi Mnyaa.
Mwaka 2005 alishika nafasi ya saba kati ya wagombea urais 10 waliojitokeza na kupata kura 21,574 sawa na asilimia 0.19, akiwa nyuma ya Mchungaji Christopher Mtikila wa DP.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anatajwa kwamba ataongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati Mchungaji Peter Simon Msigwa ataongoza Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri wa zamani wa Maliasili, Utalii na Mazingira, Juma Hamad Omar, ambaye amepitishwa na CUF kugombea katika Jimbo la Wawi kuziba nafasi ya Hamad Rashid Mohammed bado hajafikiriwa nafasi gani atapatiwa kutokana na uzoefu wake, ingawa anatajwa kwamba anafaa kuongoza Wizara ya Mazingira, lakini kashfa ya mkataba ‘haramu’ wa Loliondo inaweza kumtia doa.
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba, Juma Hamad Omar, ambaye aliongoza wizara hiyo wakati wa serikali ya awamu ya pili, hatasahaulika kirahisi katika historia ya uongozi wa wizara hiyo, kwani wakati wa uongozi wake ndipo ilipotokea kashfa ya uuzwaji wa Pori la Loliondo kwa Mwana wa Mfalme wa Falme za Kiarabu.
Kashfa hiyo ni kati ya matukio makubwa yaliyotikisa nchi kwani ilisababisha kuundwa kwa Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mateo Qaresi na chanzo cha kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wakati huo, Muhidin Ahmad Ndolanga, ambaye alimchapa kibao Qaresi bungeni pale Karimjee. Omar aliondoka katika wizara hiyo mwaka 1995 baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani.
Ifuatayo ni orodha pendekezwa ya baadhi ya wizara za sasa (japokuwa kuna uwezekano wa kuzipunguza ikiwa Ukawa wataingia madarakani ili kupunguza matumizi ya serikali):
Waziri katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora): Wilfred Muganyizi Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, ambaye kwa sasa ameshinda kura za maoni kugombea tena katika Jimbo la Bukoba Mjini.
Waziri Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma): Profesa Kulikoyela Kanalwanda Kahigi (Chadema), ambaye anagombea tena katika Jimbo la Bukombe.
Waziri katika Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu): Joseph Roman Selesini (Chadema) anatetea nafasi yake katika Jimbo la Rombo.
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): Rajab Mohammed Mbarouk (CUF) ambaye alikuwa waziri kivuli katika Bunge lililopita na anatetea nafasi yake katika Jimbo la Ole.
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi): David Ernest Silinde (Chadema), ambaye licha ya kuwa waziri kivuli katika Bunge lililopita, alionyesha umakini mkubwa hata wakati wa uwasilishaji wa bajeti kivuli. Anagombea katika Jimbo la Momba mkoani Songwe.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira): Juma Hamad Omar (CUF) anagombea katika Jimbo la Wawi.
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano): Masoud Abdallah Salim (CUF) ambaye anatetea tena nafasi yake katika Jimbo la Mtambile.
Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji): Pauline Philipo Gekul (Chadema) ndiye aliyekuwa waziri kivuli. Uwezo wake wa kujenga hoja na kuzitetea ndio umemfanya hata akashinda kura za maoni katika Jimbo la Babati Mjini mkoani Manyara.
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango: John Mnyika (Chadema), ambaye safari hii anagombea katika Jimbo jipya la Kibamba badala ya Ubungo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi: James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ambaye anagombea tena katika Jimbo la Vunjo, lakini atakumbukwa na wengi jinsi alivyoipeleka mchaka mchaka serikali Bungeni kuhusu suala la mitaala ya elimu.
Waziri wa Maliasili na Utalii: Mchungaji Peter Msigwa (Chadema). Anafahamika vyema jinsi alivyokuwa akipambana kufichua uovu katika wizara hiyo na hoja zake ndizo zilichangia wakurugenzi takriban saba wa wizara hiyo kutimuliwa.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi: Halima James Mdee (Chadema). Ni mmoja kati ya wabunge imara ambaye tangu ameingia mwaka 2005, kwanza kupitia Viti Maalum na baadaye jimboni Kawe, aliweza kufichua uozo wa serikali katika uuzaji wa ardhi na kusababisha migogoro mingi.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto: Magdalena Sakaya (CUF).
Wizara ya Katiba na Sheria: Tundu Antipas Lisu (Chadema), ndiye Mwanasheria Mkuu wa Chadema na alikuwa Mnadhimu Mkuu (Chief Whip) wa upinzani.
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko: Dk. Emmanuel John Makaidi (NLD).
Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu: Mhandisi Mohammed Habib Juma Mnyaa (CUF).
Wizara ya Kazi na Ajira: David Kafulila (NCCR-Mageuzi).

7 comments:
Angalia watu wanavyo ota ndoto ya mchana ya kujigaiwa madaraka bila hata kabla ya kuwaambia mwananchi watalifanyia nini taifa na wananchi wake. Hawa watu wapo kitamaa na uroho wa madaraka zaidi kuliko maslai ya nchi. Ukiangalia kwa makini basi hata hizo sura zao zinakuambia ni watu wenye kujali matumbo yao zaidi. Na hayo matope walio yaokota ufukweni ndio wanayaita almasi dah! Yaani wabongo kazi ipo.
Mwandishi wa makala hii hajitambui! Kutafuta ushauri unapokuwa hujui jambo fulani sio vibaya! Yumkini mwandishi hata haelewi chochote kuhusu matakwa ya Katiba ya JMT juu ya mgombea urais na mgombea mwenza wake. Vinginevyo, safu aliyotupangia isingekuwa kama alivyoiweka. Aidha, mwandishi pia hayuko current na kinachoendelea kwenye UKAWA. Vinginevyo, angemjua kwa usahihi mtu aliyependekezwa kuwa mgombea mwenza wa Fisadi!
Pamoja na kwamba mimi binafsi, I am sick and tired of CCM, sijafikia hatua ya kukata tamaa kiasi cha kuwa tayari kuiuza nchi yangu kwa genge la wahuni. I am 100% in agreement with Dr. Slaa's disapproval of this unprincipled, flip flopping behavior! Tunajua fika Lowasa ni fisadi, lakini kwa tamaa zetu tuamue kumkumbatia? No way! Mtu yeyote mwenye nia nzuri na nchi yetu hawezi kutaka kwenda Ikulu kwa gharama yoyote iwayo! Kama UKAWA tunataka mabadiliko ya kweli, why is CCMIFICATION of UKAWA necessary? Kama UKAWA tunaweza kuvutia mafisadi wengi kutoka CCM, basi sharti tujue kwamba we're going to be worse than the current administration!
Inavyoonekana wewe ni CCM uko tayari kuona ndugu zako wanaadhirika na dhiki ambayo CCM ni wao peke yao wananufaika lakini wananchi hawana hata hela ya kununua mboga. Hao waliopo hapo tayari wote wana nafasi katika vyama na bunge hawana njaa ya kula mali za wananchi ina wana hamu ya kuingia madarakani ili watatue matatizo ya wananchi. Huyu muandikaji kwanza hajui alichokiandika kwa sababu Lipumba hawezi kuwa makamo wakati bado yupo CUF.
Ccm hawakutegemea upinzani kama huu lazima wapaniki,mbona bado.
Wote ni ccm mliojifanya ni chadema mnamtetea slaa,tunaotaka madiliko hatujali nani atakuwa raisi as longer hajatoka chichiemu.
Sasa huyu Fisadi mnayemtegemea kuwa Rais wenu akishindwa kuchaguliwa, atafanya nini? Nanyi mnaotegemea safari ya matumaini mtaishia wapi? kweli mnategemea Chadema itashinda au ni ndoto tuu zilizomo vichwani mwenu? Keep on dreaming Ukawa folks, I pity you all!
haya ni maoni ya mwandishi tu,ila ametumia akili nyingi kufikiri ,nampongeza ,kikosi kiko vizuri sanaaaa ,ukawa safiiii tuwaombeee wapite tuone mabadiliko
Post a Comment