Rais jakaya Kikwete akimkabidhi irani ya ccm, mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. Mohamed Shein, wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za chama hicho uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti, mjini Unguja jioni ya leo. Picha na OMR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mgombea wa Rais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho tawala Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Urais katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mgombea wa Rais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho tawala Dkt. Ali Mohamed Shein wakionesha ilanui ya Uchaguzi ya CCM leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Urais mbele ya umati mkubwa sana katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia leo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Urais katika uwanja wa Kibandamaiti mjini Unguja.
6 comments:
Kawaida jamani tuacheni bwebwe
Mwaka huu CCM mmeshika adabu, na bado tukutane october 25
Lowasa baba ulipo tupo hata wakuchafue vipi, tutakusafisha wenyewe tarehe 25
Nyie mlie tu. Tarehe 25 Oktoba mtaiona Ikulu kwa mbali kama watalii tu pale CCM watakapotangazwa washindi.
Bahati mbaya wakati mnamsafisha mtu wenu huyo hiyo tarehe wananchi watakuwa tayari wameshatoa maamuzi ya kuirudisha CCM madarakani.
Na mjiandae kuomboleza, kwa sababu huyo fisadi wenu hana namna ya kushinda uchaguzi huu!
Post a Comment