ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 6, 2015

Curious on Tanzania Launches Tanzania Culture Fest in New York City iliyofanyika September 5, 2015 yafanikiwa vizuri

 Curious on Tanzania Launches Tanzania Culture Fest in New York City  iliyofanyika September 5, 2015 ndani ya ukumbi wa Punto Space New York City yafanikiwa vizuri katika show hiyo kulikuwa na Chakula, ngoma nyote vyenye asili ya Kitanzania pia kulikuwa na Arts zilizochorwa na Jojo Hassan. Chakula cha Kitanzania kilipikwa na wataalamu wa mankuli ya Kitanzania Mzee Lukas na James. Show hii ilindaliwa na mwanadada wa Kitanzania anaejulika kwa jina la Justa Lujwangana na kudhaminiwa na wadhamini mbali mbali hili kufanikisha mpango mzima ukumbini hapo. Justa ni Founder wa Curious on Tanzania.Ukitaka kujua Curious on Tanzania ni nini jitiririshe kwa kukandamiza hapa kiroho safi, http://www.curiousontanzania.com . Sasa ni wakati wa kujitiririshe hapa chini kujionea mambo yalinogaje ndani ya ukumbi huo wa Punto Space.

Warembo wakijimwaga na ngoma yenye asili ya Tanzania ukumbini hapo hakika sakafu hii kama ingekuwa udogo kama kule kwetu Ikwiriri basi vumbi lingetimka maana wadada awa walicheza na nguvu na majojo ya kiufundi kucheza ili goma.


Justa Lujwangana ndiyo kinala wa mpango mzima uliosababisha watu mbalimbali kukutana ukumbini hapo na kufurahi kwa chakula na ngoma za asili ya Tanzania,  hapo  Justa akitangulia shukrani na pongezi kwa watu  wote
waliojitokeza na kufanikisha mpango mzima kwa siku hiyo ya jumamosi ya tarehe 05. Kwakweli Justa anaitaji pongezi kwa kujiongeza kwa namna moja au nyingine kuitangaza Tanzania na vivutio nyake vya asili.
Hapa ni mmoja ya wadhamini wa shughuli hiyo kutoka kampuni ya ndege ya Delta akiongea machache ukumbini hapo.

Miss Tanzania USA alikuwepo pia kuchagiza yale yote yaliyoendelea ukumbini hapo hapa akiongea.
Mdada wa Kitanzania akiimba wimbo wa malaika kwa ukimbini hapo.


Bendi live ndiyo ilikuwa ikitoa burudani kwa watu wa mataifa mbalimbali waliojitokeza ukumbini hapo, Kwa picha zaidi basi jitiririshe hapa chini kwa kukandanimiza soma zaidi.



No comments: