ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 6, 2015

KAMPUNI YA UREMBO YA MARY KAY, YATOA DARASA KWA WAFANYAKAZI WA KIKE WA VODACOM KUHUSU MATUMIZI YA VIPODOZI

Mshauri wa kitaalamu wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya (Mary Kay) Jacqueline Macha(kulia)akimremba Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu , Vodacom Tanzania,Joan Makwai,wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania,mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakichagua vipodozi mbalimbali vya kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo (Mary Kay) wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kujiremba kwa kutumia vipodozi hivyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya kampuni hiyo mahususi kwa wafanyakazi wake.
Jacqueline Macha ambaye ni mshauri wa kitaalamu wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya Mary Kay akiwaonesha wafanyakazi wa Vodacom Tanzania moja ya picha iliyorembwa kwa kutumia vipodozi vya kampuni hiyo wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi hivyo.Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Vodacom Tanzania,Joan Makwai (kulia) akimsikiliza kwa makini Jacqueline Macha ambaye ni mshauri wa kitaalamu wa kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya Mary Kay akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo .Mafunzo hayo yaliandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya kampuni hiyo mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyaka wa Vodacom Tanzania walioshiriki katika mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo ya Mary Kay,wakimsikiliza Mshauri wa kitaalamu wa kampuni hiyo Jacqueline Macha,wakati wa mafunzo mafupi ya jinsi ya kutumia vipodozi vya kampuni hiyo yaliyoandaliwa na Idara ya Rasilimali watu ya Vodacom Tanzania,mahususi kwa wafanyakazi wake jijini Dar es Salaam.

2 comments:

Anonymous said...

Huyu dada anauza huo vipodozi vya Mary Kay yeye mwenyewe havitumii nini? Sura yake haionyeshi kama anatumia hivyo vipodozi utazani anakaa bongo. Watu wanaouza vipodozi vya Mary Kay huwa wanavutia sana na wanavaa vizuri kibiashara. Anaiga kuvaa jeans za kuchanika nywele,body no vipodozi siyo sawa. Hao madada wa vodacom wako vizuri kuliko yeye na wabongo kwa ulimbukeni wanapachikwa mabei ya kufa mtu sababu vimetoka Marekani.

Anonymous said...

Kwa hiyo we anon9.08pm unataka kusema unamfahamu huyu dada zaidi ya kusoma hapa? Kama sio unajua je kama anatumia MK lakini ngozi yake haijakubali? Au kama anatatizo fulani la afya linasababisha ngozi isikubali kama wengine? Kuhusu mavazi mi sionI tatizo personalities zinatofautiana. Unless one has all the facts tusikimbilie ku-judge wengine.