Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia) akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai baada ya kujiunga na Chadema hivi karibuni. Kushoto ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Segerea, Makongoro Mahanga. Picha ya Maktaba
Ingawa ilitokana na ulimi kuteleza, yeye mwenyewe alisema alitamka neno CCM kama utani ili kubaini ni wananchi wangapi wanaokishabikia chama hicho kati ya waliojitokeza uwanjani hapo kumsikiliza wakati tayari amekwishaeleza jinsi chama hicho tawala kilivyoshindwa kuliletea taifa maendeleo.
Msindai kama Lowassa
Wakati Lowassa akieleza kwamba alisema hayo kwa utani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai aliyekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, alitoa mpya baada ya kukiombea kura chama chake hicho cha zamani badala ya Ukawa kwenye mkutano wa hadhara.
Msindai alitoa mpya hiyo juzi jioni wakati akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni Jimbo la Manyoni Magharibi na Mashariki uliofanyika Manyoni mjini kwa tiketi ya Ukawa.
Baada ya kuwanadi wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa majimbo hayo, Msindai ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM Tanzania, aliwaomba wakazi wa Manyoni akisema:
“Mpeni kura Lowassa ni mchapakazi na mwadilifu, anauchukia umaskini ataikomboa nchi yetu na kura zote za Rais, wabunge na madiwani wapeni wagombea wa Chama cha Mapinduzi.”
Baada ya tamko hilo, uwanja ulilipuka kwa kelele na minong’ono ndipo kiongozi mmoja aliponyanyuka na kwenda alipokuwa Msindai ameketi na ni kama alimwambia: “Hapa ni Ukawa si CCM.”
Alipopata maelekezo hayo, Msindai alisimama na kusema: “Ninaomba radhi, unajua koo limekauka, hebu kwanza naomba mnipe maji nipooze koo.”
Alipoletewa maji na kuyanywa, aliendelea kuomba radhi na kusema: “Ndugu zangu, ulimi uliteleza... si mnajua tumetoka huko hivi karibuni Uccm haujatutoka sawasawa,” alisema na kuamsha kicheko kwa mashabiki waliokuwa wakimsikiliza.
Akizungumza kwa simu jana, Msindai alikiri kuombea kura wagombea wa CCM kwenye mkutano wa Ukawa lakini alisema kuwa ulimi uliteleza na kwamba aliomba radhi na watu walimwelewa.
Hata hivyo, Msindai alikazia kusema kuwa Watanzania wanataka mabadiliko kwani hata mgombea wa CCM, Dk John Magufuli katika hotuba zake amekuwa akisema anataka kuona Tanzania ikibadilika.
“Watanzania watabadilika ikiwa Dk Magufuli atatimua watu wote kwenye mfumo wa utawala na kuleta mabadiliko ya kweli, lakini kama watu watabakia walewale, watamwangusha,” alisema Msindai.
Alipoulizwa utayari wa Watanzania kubadilika, Msindai alisema Ukawa ndiyo watakaoleta mabadiliko ya kweli kwa kuwa watawaondosha watu wote na kuleta watu wapya kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema.
Alisema CCM ya sasa siyo ile ya (Julius) Nyerere na imebadilika na haitumikii tena wananchi na kwamba, Dk Magufuli ni mwenye hasira hivyo anakosa sifa.
Mmoja wa makada wa Chadema Mkoa wa Singida, Paschal Mlaki alieleza kushangazwa na kuteleza kwa Msindai akisema ana wasiwasi na waliokuja kwenye chama hicho. “Mimi ni kada wa Chadema hapa Singida, hakuna asiyenijua, ukweli hili limetukwaza wengi... hivi inaingia akilini kweli uko mkutano wa Ukawa ukatangaza CCM?
“Watu wanatumia gharama zao kufanya maandalizi, wanataka kupata vitu vya Ukawa halafu anakuja kututangazia haya!”
MWANANCHI
4 comments:
Ukawa mpo position nzuri tu, yaa wahamiaji wafanyieni subira kidogo. Ni wanadamu wa kawaida na wanaweza kuteleza. Your change message is sinking to the voter.
Nawapa kudos, na mtashinda October 25 kwa ushindi mnono tu. Anytime mkiona J.K anapanda jukwaani mjue hali ya upande wa pili ni mbaya, wanakaa kila mara na wanafanya tafakur na wanapatwa na jazba. CCM is on falling anxiety, desparate and cant convinced the voters in any shape or form. Now they are resorting to using their celebrity outgoing chairman to pull the mass on campains, and that is even a deadly move than letting Magufuli mentioning his tasks on his previous assignments.
Kwishney the green party.
Nonsense! I hate people who try to write in a language they functionally are unable to effectively use to communicate their views. This ain't anything other than unproductive aggrandizement!
Mbabaishaji kamwe haachi kubabaika hao ukawa ni wababaishaji wakubwa na hao wagombea wao ni wababaishaji wakubwa hakuna kipya watakachowaletea watanzania zaidi ya kujinufaisha wao wenywewe na familia zao na wanaoendelea kudanganywa na hao wababaishaji waendelee kufanya hivyo lakini hapo pa ukawa hapana kitu pumba tu. Na hao wagombea wao wameshaanza kujichanganya kwa kuipigia debe CCM si walaumu mziki wa magufuli si mchezo lazima wachanganyikiwe.
You better hate yourself. kwanini useme hivyo hujioni kuwa na wewe ni tatizo.
Post a Comment