Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad akiwahutubia wajumbe wa Kamati za Ushindi za Wanawake wa CUF
kutoka Wilaya nne za Pemba huko skuli ya Fidel Castro.
Wajumbe wa Kamatui za Ushindi za
Wanawake kisiwani Pemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hanmad mara baada ya kuzindua kamati hizo
huko skuli ya Fidel Castro mkoa wa Kuisni Pemba.
Na. OMKR Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad leo amezindua Kamati za Ushindi za
Wanawake Kisiwani Pemba na kuwahimiza wajumbe wake kufanya kazi kwa
bidii kukihakikishia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu wa
mwezi Oktoba.
Akihutubia katika hafla ya uzinduzi huo
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano skuli ya Fidel Castro, mkoa wa
Kusini Pemba, Maalim Seif amesema wanawake wana uwezo mkubwa wa
kuwafikia wapiga kura popote pale walipo.
Amesema mchango wa wanawake katika
uchaguzi ni wa kipekee na wamekuwa kama askari wanaoweza kutumwa
sehemu yoyote ile na kwenda kufanya kazi kwa mafanikio makubwa.
Amewataka wanawake wa CUF katika
kufanya kazi hiyo wawe na hekima na busara na wawafikie wanachama wa
vyama vyote wawaeleze mipango na mikakati mizuri ya CUF katika
kuwaletea maendeleo wananchi pale kitakapo kamata Serikali.
Naibu Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya
Wanawake CUF, Mhe. Zahra Ali Hamad amesema wajumbe hao wa Kamati za
Ushindi wako tayari kutumia ushawishi walio nao kwa kupita nyumba
hadi nyumba kuwahamasisha wanawake wenzao na vijana kukipa kura
nyingi chama hicho.
Mapema katika risala ya Kamati hizo
iliyosomwa na Bimkunga Hamad wamesema wamejipanga vizuri kuhakikisha
wanawapatia kura na ushindi wa kihistoria wagombea Urais, Edward
Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad kupitia ushirikiano wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Khamis Haji, OMKR
No comments:
Post a Comment