Makamu Mwenyekiti wa Mpira wa Mikono Zanzibar (BAZA) Ramadhani Khamis Salmin akizungumza wakati wa ufunguzi huu wa michuano ya Kombe la Karume Cup uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar na kushirikisha timu 17 za mchezo huo kwa Zanzibar 6 zikiwa za Wanawake na 11 za Wanaume.
Mlezi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Mama Shadya Karume akitowa shukarani zake kwa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (BAZA) kufanikisha michuano hiyo kwa kipindi chote cha miaka 12 kwa kumuezi Mzee Abeid Amani Karume na kutowa shukrani kwa mbunifu wa michuano hiyo. na kuipongeza (BAZA) kwa ushirikiano unaoonesha katika kuendeleza michuani hiyo ya Kombe la Karume Cup.hii ni michuano ya 12 tangu kuazishwa kwake.
Mlezi wa Michuano ya Kombe la Karume Cup Mama Shadya Karume akiwa na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar (BAZA) akiwasili katika viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya ufunguzi wa Michuano hiyo ya 12 ya Karume Cup tangu kuazisha.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mareheme Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume akisalimiana na Viongozi wa Michezo Zanzibar wakati akiwasili katika viwanja vya Gymkhana kwa ajili ya kufungua Michuano ya 12 ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi Ball, akiwa mgeni rasmin wa michuano hiyo inayoshirikisha timu 17 za Wanawake inashirikisha timu 6 na Wanaume inashirikisha timu 11.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sharifa Khamis (Shery) wakati akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya Karume Cup kwa mchezo wa Basketi Ball.
Mama Fatma Karume akisalimiana na Mjuu wake Ahmeid Abeid Karume wakati akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya ufunguzi wa michuano hiyo.
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball) uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar
Washiriki wa Michuano ya Karume Cup wakiingia uwanjani kwa maandamano kwa ajili ya Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono (Basketi Ball) uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar
Mgeni Rasmin wa Ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Mikono Zanzibar Mama Fatma Karume akizungumza na Wanamichezo wakati wa ufunguzi huo uliofanyika katika viwanja vya gymkhana Zanzibar na kuwataka Vijana kuendelea kukuza mchezo huo na michezo ni afya. na kuwaasa Vijana kuendeleza michezo.
Baadhi ya wapenzi wa mchezo wa Basketi wakiwa katika viwanja vya gymkhana wakifuatilia ufunguzi huo.
Baadhi ya Viongozi wakimsikiliza Mama Fatma Karume akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo wakati wa ufunguzi wa michuano ya Karume Cup Zanzibar.
Timu washiriki wa michuano ya Karume Cup wakimsikiliza Mama Fatma Karume akitowa nasaha zake kwa wanamichezo hao wakati wa ufunguzi wa michuano ya Karume Cup yaliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar
Mama Fatma Karume akiongozana na Viongozi wa (BAZA) kwenda kuzindua michuano hiyo kwa kurusha mpira golini kuashiria kuzindua michuano hiyo.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume akizundua michuano ya Mpira wa Mikono (Basket Ball) Kombe la Karume Cup katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, akirusha mpira kufunga basketi wakati wa uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment