ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 12, 2015

MBASHA, GWAJIMA KIMENUKA UPYA!

gwajima.jpg

Brighton Masalu

NI kweli kimenuka! Siku chache baada ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kujibu mapigo ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, sasa kimenuka upya, Risasi Jumamosi linakupa zaidi!

Kimenuka kwa nani? Ni kwa Emmanuel Mbasha ambaye ni mume aliyetengana na mkewe, Flora Mbasha huku mwanaume huyo akisimamia madai yake kwamba, Gwajima alisimamia mchakato mzima wa yeye na mkewe kutengana.

AIBUKA UPYA


Akizungumza na Risasi Jumamosi katika mahojiano ya takribani dakika thelathini juzi jijini Dar, Mbasha alisema alimshuhudia Gwajima, Jumanne wiki hii akitupa shutuma kwa Dk. Slaa tena kwa kuyaanika mambo yake ya ndoa, yeye akashangaa sana.

“Na mimi leo nataka kumjibu Gwajima kama yeye naye alivyojitokeza kumjibu Dk. Slaa. Gwajima niliwahi kumshutumu kwa kuhusika na kuvunjika kwa ndoa yangu. Leo hii anasimama kwa kujigamba akisema Slaa si msafi, yeye ana usafi gani?.

AFICHUA SIRI MPYA


“Lakini kiko wapi sasa! Hata huyo Flora mwenyewe ameshamkimbia, yuko kwingine. Kwa hiyo kama ishu ni uchafu, Gwajima pia si msafi. Ana mambo anajua alikuwa akiyafanya kwa mke wangu, mimi nayajua na nina ushahidi.”

Hata hivyo, Mbasha hakufafanua, Flora amemkimbia Gwajima kivipi? Na huko kwingine alikokwenda ni kwa nani na kwa sababu gani!

ANA MAZITO YA GWAJIMA

Lakini alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Naomba leo niseme kwamba nina mambo mazito sana ya Gwajima

ambayo siku ikifika nikienda kuyasema kanisani kwake waumini wake watashangaa wote. Muda bado haujafika lakini ukifika nitamlipua.”

Risasi Jumamosi: “Je, kuibuka kwako upya tukisema umetumwa na chama kimoja cha siasa umchafue Gwajima, utasemaje?”

Mbasha: “Kwani ye’ alitumwa na nani? Mimi nimeibuka kwa sababu hata yeye ameibuka. Kama angesimama pale (Ukumbi wa Hoteli ya Landmark) akasema mambo yake bila kukosoa ndoa ya Dk. Slaa hata mimi nisingepanua kinywa kusema. Hawezi kusema siri za mwenzake kama mtumishi. Tena anasema mpaka ishu ya Dk. Slaa kulala ndani ya gari.”

“Nimeamua kusema kwa sababu yeye amemwona mwenzake si msafi. Yeye usafi wake ni upi? Niliachana na Flora, akaenda kwake, yeye akampokea. Angekuwa msafi angemshauri Flora kwamba alichofanya si kizuri. Hapo ningesema ni msafi.”

AMKUMBUSHA GWAJIMA KUHUSU MOROGORO

“Gwajima akumbuke kabla ya ukaribu wetu haujafa, mimi, Flora na yeye tulikwenda Morogoro kwa ajili ya huduma ya Mungu. Nini kilitokea? Lakini sijasema. Ajitokeze anijibu na mimi halafu nitasema nini kilitokea. Kwa sasa sitoi risasi zote, nasubiri ajibu.”

NDANI YA MITANDAO

Ndani ya mitandao mbalimbali ya kijamii, majibu ya Gwajima kwa Dk. Slaa yamekuwa gumzo. Timu ya Mbasha imemtupia shutuma kali Gwajima ikikumbushia mgogoro wa Flora na mumewe huku kundi jingine la Gwajima likitetea kuwa, hakuna uhusiano wowote wa mgogoro wa Mbasha na mkewe na majibu ya Gwajima kwa Dk. Slaa.

GWAJIMA SASA

Juzi, gazeti hili lilimsaka kwa njia ya simu Mchungaji Gwajima ili aweze kujibu shutuma za Mbasha ambazo ni kama ameziibua upya lakini simu yake haikuwa hewani.

Hata hivyo, katika mkutano wake na wanahabari Jumanne, Gwajima alisema: “…kwa hiyo Dk. Slaa si msafi. Dk. Slaa huyu wa leo si yule wa mwaka mmoja uliopita! Lakini ukiangalia kwa makini sana, si yeye, matatizo yapo kwa yule mke wake, amemkamata.”

Pia, Gwajima alianika siri akidai kuwa, Dk. Slaa aliwahi kutupiwa virago nje akalala kwenye gari baada ya kubaini kuwa, ameridhia, Chadema kumpokea waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kugombea urais.

FLORA NAYE ANA MAMBO MENGI

Wakati Mbasha akirusha madai hayo huku akisema mkewe amemkimbia Gwajima na yuko kwingine, kwa upande wake, Flora aliwahi kusema: “Nina mambo kibao ya Mbasha, nikiyasema watu

watashangaa! Lakini siku zote mimi namwachia Mungu tu. Yeye ndiye muweza wa yote.”

MKE WA DOKTA SLAA

Kuhusu madai ya kumfukuza mumewe nje na kulala kwenye gari, mke wa Dk. Slaa, Josephine Mushumbuzi aliwahi kusema: “Najiuliza nini

kinaendelea, kuna mambo mwanamke huwezi kumfanyia mwanaume. Mume atabaki kuwa mume tu siku zote.”

SLAA AHOFIA

Kuhusu madai ya kukatiliwa kuingia ndani ya nyumba na mkewe na kulala ndani ya gari, Dk. Slaa alipoulizwa kihabari, alisema: “Mambo hayo ni ya kifamilia sana. Sitaki tu kuzungumzia mambo ya familia za watu nikiyasema utatokea mpasuko! Tuache tu.”

GPL

2 comments:

Anonymous said...

Ccm kila kona askofu tema yote tujuwe
Na chaguo letu Lowassa
Lowassa
Lowassa

Anonymous said...

Mbasha alibaka shemeji yake ambaye ni mdogo kiumri ndiyo kilisababisha kuachana na Flora hata mahakama ilidhibitisha hivyo. Huyu jamaa anielezi kitu nikamwamini alifanya kitu ambacho binadamu wa kawaida asingefanya. Najua anataka leta shutuma eti Gwajima amezaa na Flora huo ni kuudhalilisha uwanaume wako mwenyewe tafuta maisha mengine na utubu kwa mwenyezi Mungu kwa uasherati