ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 5, 2015

Reggae Time ya Pride FM......Justin Kalikawe

Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.
Kwangu ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu. Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).
Na nakumbuka tulipanga kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. Ni katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi. Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.
Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwisho wa ushiriki wake katika mkakati huo.
Lakini wakati anafariki, nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.
Lakini….
Justin Kalikawe ni nani?

No comments: