Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars imetoka suluhu ya 0-0 na Timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles katika mchezo uliochezwa leo Jumamosi Sept 5, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo ambayo matangazo yake yalinaswa na Vijimambo Blog kupitia tunein ya Radio E- FM, Taifa Stars inastahili pongezi kwa kiwango cha mpira ilichokionesha leo bila kujali ni timu gani au ukubwa wa timu waliocheza nayo.
Kutokana na matangazo ya Radio hiyo yaliyoletwa moja kwa moja kutoka uwanja wa Taifa timu ya Taifa Stars ilicheza vizuri muda wote na walipiga mashuti matano ya hatari langoni mwa timu yenye jina kubwa katika historia ya soka Duniani kitu kilichoelezewa na watangazaji hao kwamba ni jambo la kujivunia na kumwagia sifa kocha wa timu hiyo Charles Mkwasa kwa kubadilisha timu hiyo ilichocheza mpira wa kiwango cha juu.
Kitu kingine watangazaji hao walichosifia kuhussu kocha huyo ni kuusoma mchezo na kufanya mabadiliko yaliyoongezea nguvu Taifa Stars. Mpaka dakika 90 Taifa Stars 0 Super Eagle 0.
1 comment:
Sio matekeo mabaya ukilinganisha na uchanga wa benchi la ufundi. Pongezi kwa benchi lote la ufundi kwa mara ya kwanza kwa muda wa kipindi kirefu vijana wamefanya kazi uwanjani kwa kuonyesha uzalendo hasa ni vitu vya kujivunia. . Masisitizo kwa benchi la ufundi jithada ifanyike vijana wapatiwe mechi za kutosha za kujipima nguvu. Vilevile inatupasa kuacha mazoea ya kujipima nguvu na nchi zenye viwango hafifu . Kila kitu cha dunia ya leo ni cha ushindani hasa na huwezi kuwa mshindani kama hujashindana na anaekushinda ukamshinda. Jambo jengine benchi la ufundi liache kupanga wachezaji kwa mazoea ya majina kwa mfano sub iliofanywa ya John Boko haikuwa sahihi . Kijana kama Rashid mandawa ingekuwa surprise tosha kwa wanaegiria.
Post a Comment