Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora) wametakiwa kuwa kichocheo cha
kuleta maendeleo ya biashara na uwekezaji katika nchi yao ili kuongeza pato la
taifa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Kauli hiyo imetolewa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula wakati wa kufungua kongamano la wafanyabiashara linalofanyika Birmingham, Uingereza tarehe 4 na 5 Septemba 2015.
Aliwaasa washiriki wa kongamano hilo kulitumia kama jukwaa la kufanya
majadiliano kwa madhumuni ya kubadilishana mawazo mapya ili kuibua fursa
lukuki za uwekezaji nchini Tanzania. Aidha, aliwahimiza wanadiaspora kushirikiana na wajasiliamali wa nyumbani ili kuzitumia fursa hizo ipasavyo.
|
1 comment:
Kwanini mnatunyima uraia pacha sasa....?? Watanzania unafiki unaturudisha nyuma sana. ..
Post a Comment