ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 17, 2015

AECF KUENDESHA SHINDANO LA UFADHILI WA BILIONI 17 KWA MAKAMPUNI YA KILIMO NA BIASHARA

 Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi AECF, Hugh Scott akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati akizungumzia shindano litakaloshirikisha kampuni za Tanzania zinazojishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ambalo litafanyika hapa nchini  shirika ilo linalojishughulisha na mikopo ya shughuli za kilimo na biashara hapa nchini Tanzania.
 Mkuu wa Huduma za Shirika la AECF, Bw.Sam Sang’ang’a  akizungumzia kuhusu mashindao yatakavyofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo leo jijini Dar.
Waandishi wa habari wakiendelea kuchukua habari katika ukumbi wa Habari maelezo jijni Dar ambapo Mfuko wa Sekta Binafsi AECF ulikuwa unatanatangaza mashindano kwa makampuni yatakayonufaika na mkopo wa Bilioni 17.


 Na Nyakongo Manyama – Maelezo 
Serikali ya Uingereza kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya nchi hiyo imetoa shilingi bilioni 17 kwa ajili ya shindano la ufadhili wa kilimo cha biashara na huduma za kifedha hapa nchini. 

Shindano hilo la awamu ya nne linalosimamiwa na Mfuko wa Sekta binafsi (AECF) lina lengo la kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo cha biashara na huduma za kifedha vijijini na kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa soko nchini. 
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugezi wa AECF Hugh Scott alisema mtazamo wake ni kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania katika soko hilo kwa kuipa changamoto sekta binafsi. 
“Natazamia kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania katika shindano hili kwa kuipa changamoto sekta binafsi kuchangamkia fursa iliyotolewa na mfuko wa EACF na kuitika kwa kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya watanzania waishio vijijini”, alisema Scott. 
Scott aliendelea kusema shindano hilo lipo wazi kwa kampuni zinazotengeneza faida ya ndani na ya kigeni yenye lengo la kufanya kazi na kuimarisha sekta ya kilimo cha biashara pamoja na kupata ufumbuzi utakaoongeza huduma za kifedha vijijini na taarifa katika kusaidia uzalishaji katika kilimo cha biashara Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. 



Kwa upande wake Sam Ng’ang’a ambaye ni Afisa Mkuu anayeshughulikia uendeshaji katika mfuko huo aliyataja mambo ya kuzingatia wakati wa utumaji wa maombi kuwa ni pamoja na uwezo wa kampuni katika kutekeleza mradi, ubora wa wazo la kibiashara manufaa kwa jamii pamoja na ubunifu. 



Hili ni shindano la nne kufanyika hapa nchini awamu ya kwanza ilianza mwaka 2011 ambapo hadi sasa jumla na kampuni 37 zilliidhinishwa kupata ufadhili huo.

No comments: