ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 17, 2015

BREAKING NEWS: JOB NDUGAI NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA




Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Goodluck Ole Medeye ambaye amepata kura 109.

Hata hivyo wagombea hao ambao walikuwa 7 kati ya 8 wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa Ndugai wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na kumtaka aongoze vyema bunge hilo.

 Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365


Matokeo ya kura za Spika.


A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0

F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0

Kura zilizoharibika ni 2

3 comments:

Anonymous said...

Huyu mpigana ndondi mtaani leo spika ?

Anonymous said...

Huyu jamaa anapiga watu mtaani na pia alifungliwa RB imefutwa.?.convict or possible convict.?..h

Anonymous said...

Cha ajabu ni nini? Mbona aliyekuwa mwana mieleka (former professional wrestler) wa Kimarekani kwa jina Jesse Ventura alichaguliwa na kushika wadhifa wa Gavana wa State ya Minnesota (Marekani) tarehe 3 Novemba, 1998?