Tuesday, November 24, 2015

DR SHEIN NA MAALIM SEIF KUKUTANA TENA LEO KWA MARA YA TATU

Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, yataendelea kufanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Mazungumzo ya kikao hicho ambacho ni cha tatu, kitaongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
Wajumbe wa kikao hicho ni Marais wastaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amani Abeid Karume, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mazungumzo hayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), kufuta matokeoi ya Uchaguzi Mkuu visiwani humu Oktoba 28, mwaka huuu na kuibua mgogoro mkubwa wa Kikatiba.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, amesema kuwa hadi sasa mazungumzo hayo bado siri kubwa hata viongozi wa ndani ya chama chake, hawafahamu kinachoendelea tangu viongozi hao wa kitaifa kuanza kukutana.


Amesema inasikitisha mno vikao vyote vitatu vilivyofanyika pamoja na hicho kinachotarajiwa kufanyika leo, upande mmoja unawakilishwa na watu watano wakati upande mwingine ukiwa na uwakilishi wa Maalim Seif peke yake.

Amedai kuwa mashariti yaliyowekwa katika muongozo wa mazungumzo, ni magumu kwa kuwa hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi wa Zanzibar zaidi ya Maalim Seif pekee.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake