POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yaliyopangwa kufanyika bila ukomo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kinyume cha sheria.
Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, kwamba maandamano hayo yana viashiria vya uvunjifu wa amani.
Maandamano hayo yaliyotajwa kuwa hayana kikomo, yalipangwa kufanyika katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam. Kova alisema kama yakiruhusiwa, yatakuwa chanzo cha mfarakano mkubwa nchini, jambo ambalo litaathiri amani na maisha ya Watanzania.
Alisema maandamano hayo ni jambo ambalo haliwezekani, kwani pia yatasababisha msongamano mkubwa kwa wakazi wa jiji hilo na watapata usumbufu kwa kushindwa kufanya shughuli zao kwa ufasaha.
Alisema walipokea barua yenye Kumbukumbu namba CDM/PW/ GEN/042/2015 iliyoandikwa Oktoba 31, lakini iliwasilishwa ofisini kwake jana, ikitoa taarifa ya kufanya maandamano leo.
“Katika barua hiyo, Chadema Kanda ya Pwani walitoa taarifa ya kufanya maandamano ya amani yasiyo na kikomo kuanzia kesho (leo) katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam kupinga kile walichodai ni uporwaji wa demokrasia dhidi ya mgombea wao wa urais Edward Lowassa ambaye wamedai ndiye mshindi,” alisema Kova.
Alisema baada ya kusoma barua hiyo kwa makini na kutafakari, amebaini kuwa kutokana na Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322 Kifungu cha 43 (1) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002, taarifa ya maandamano inatakaiwa itolewe saa 48 kabla ya muda wa kuanza maandamano, kitu ambacho kimekiukwa, kwani barua hiyo ilipelekwa ofisini kwake jana.
“Kwa mujibu wa sheria hii, Chadema hawataruhusiwa kufanya maandamano hayo kutokana na kuchelewa kutoa taarifa kwa wakati. Wamemtaja Lowassa kuwa ndiyo mshindi, lakini kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndiyo ina mamlaka ya kumtangaza mshindi,” alisema.
Alisema maandamano hayo ni batili na ni kinyume cha Sheria. Alisema kama hawakuridhika na uamuzi huo wa polisi, wanaruhusiwa kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi chini ya Kifungu Namba 43 (6) ya Sheria za Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322.
Hata hivyo, Kova alisema barua hiyo iliyowasilishwa na Chadema imeandikwa huku ikitawaliwa na shari; na pia inaonekana taarifa hiyo lengo lake ni kuvuruga amani.
“Nawaomba viongozi wa Chadema watumie busara, wasitake kuiingiza hii nchi katika matatizo na umwagaji damu, Watanzania sisi ni watu wa amani, hatujazoea haya mambo. Kuna taratibu na sheria wazifuate hizo,” alisema.
Alisema polisi wamejipanga vizuri kuhakikisha nchi inakuwa salama na atakayekaidi agizo hilo, atachukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, alitaka vijana wasikubali kutumiwa katika kuvuruga amani.
HABARI LEO
Hao wapuuzi wamedhamiria kufanya vurugu yatakayoleta maafa makubwa Tanzania. Uchaguzi umekwisha kuna mambo kibao ya msingi ya kukifanyia chama chao ili kiwe cha upinzani wa kweli kwa mfano kila mtanzania anajua kuwa chadema ni chama kilicho kumbatia ukanda. Kwa hivyo huu ni wakati muufaka kwa Chadema kukisafisha chama chao na tuhuma hizo nzito baadala ya kuendelea kujenga taswira kwa watanzania ya kuwa watu kutoka semu moja ya nchi wana mikakati ya kuimiliki nchi zima hata ikiwa kwa mabavu. Kwa mfano Vyombo vya habari vingi vinavyomshabikia chadema na lowasa hufanya hivyo zaidi kwa kasumba ya ukanda ni ukweli usio pingika hata tukikanusha.
ReplyDeleteMaandamano hayata wasaidia chadema kufanikisha kitu chochote cha maana , zaidi ya kuwapootezea wananchi hali ya utilivu na amani katika shughuli zao za kila siku.
Hawa wazee wa Chadema wanataka kuwapotosha watoto zetu. Wao wanayo plan B, just in case mambo yatawaendea vibaya, watapanda ndege na kutoroka. Vile vile wao wanazopesa za kuweka dhamana wakiwekwa mbaroni. Jee? nani atawadhamini hawa vijana wakitiwa mbaroni? Lakini, hamuoni kuwa mnapoteza muda kuandamana bila faida? The only possible outcomes from the so-called demonstrations is bloodshed. Who want that?
ReplyDeletenimezisoma sababu zako kamanda kova na kuziona ni za kitoto mno,hazina uzito na kwa watu walio makini wanakuona HUFAI,HOVYO.unazungumzia msongamano.hivi kweli kova ni wewe kova ninayekufahamu siku zote?unaelewa,huelewi kwamba katika majimbo kumi ya uchaguzi mkoa wa dar-es-salaam majimbo sita[zaidi ya nusu]yamechukuliwa na ukawa.dar ina wakazi wapatao million tano,sasa huo msogamano wa wana ukawa unaokupa jinamizi ni lini unadhani utapungua ili utoe ruhusa.kwanza wewe kama nani kutuzuia tunapoamua kuandamana?wewe nani?nakuuliza tena wewe nani.nakwambia kova,wananchi tumedhulumiwa na tunapoamua kuandamana tunataka dunia itusikie kilio chetu,pili tunawaambia waliotuibia ushindi kwamba ushindi wetu upo pale pale.kova jiepushe kutumiwa na ccm unatia aibu,aibu kubwa.
ReplyDeletechadema wapande ndege na kutoroka?ABSURD.au ulikua una maana ya rais anayesaafu alhamisi tarehe 5 novemba jakaya mrisho kikwete,maana yake kwa leo kuna kiila dalili kwamba rais mpya mhe.john pombe magufuli atamfikisha kwenye vyombo vya dola kwa kosa moja kubwa MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA-OFISI-subiri utakuja sikia.siku si nyingi,kwanza mheshimiwa aingie ofisini ajionee.
ReplyDeleteWakati wa kampeni za uchaguzi hawa ndugu zetu walikuwa wanaongelea kupeleka viongozi mbalimbali wakiwemo wa usalama wa taifa kwenye Mahakama Ya Kimataifa huko Uholanzi. Mimi nadhani wao ndiyo walikuwa wanaomba kijanja kupelekwe kwenye Mahakama hiyo kwa ajili vitendo vyao sasa vinaonyesha kuwa wanastahili kuweko huko.
ReplyDeleteACHA UNAFIKI,ACHA UCHOCHEZI. ACHA UONGO.UKAWA HAINA MATATIZO YEYOTE WALA AGENDA ILIYOJIFICHA NA VYOMBO VYOTE VYA DOLA.POLISI NI RAFIKI WA UKAWA,USALAMA NI RAFIKI WA UKAWA,MAJESHI NI RAFIKI WA UKAWA.USICHANGANYE BAADHI YA WATOA AMRI WALIOMO NDANI YA HIVI VYOMBO [MFANO KOVA,CHAGONJA,TUMSIME,MSANGI] AMBAO DHAHIRI NI WANA CCM KATIKA UNIFORM.] HAWA,UKAWA ITAWASHITAKI MAHAKAMANI NA KWA KUWA USHAHIDI UPO DHIDI YAO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE [NDANI YA TANZANIA]
ReplyDelete