Monday, November 23, 2015

Mugabe kutafutiwa kiti cha magurudumu


Image copyrightGettyImage captionRais Robert Mugabe wa Zimbabwe na mkewe Grace.

Mkewe rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ,Grace, amekanusha madai kuwa anapania kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao kumrithi Mugabe ambaye ana umri wa miaka 91.

Grace badala yake ameapa kufanya kila awezalo kufanikisha uongozi wa Mugabe ''hata ikiwa ni kumsukuma kwa kiti maalum cha magurudumu''
'Nimesimama hapa mbele yenu kama mkewe rais Mugabe wala sina haja na wadhfa mwengine'. alisema Grace

Katika mkutano huo wa hadhara uliohudhuriwa na wafuasi wa ZANU PF , Grace aliahidi kumtafutia mumewe kiti maalum cha magurudumu.

''Hata hikiwa itanibidi nimtafutie kiti maalum cha magurudumu nitamtafutia''Image copyrightBBC World ServiceImage captionGrace ameapa kufanya kila awezalo kufanikisha uongozi wa Mugabe ''hata ikiwa ni kumsukuma kwa kiti maalum cha magurudumu''

''Nitaisukuma mwenyewe kumpeleka akatekeleze wajibu wake wa kuiongoza Zimbabwe na hata kupiga kura alisema Grace mwenye umri wa miaka 50.

Nitahakikisha anaongoza maadam anaweza kuzungumza na watu wake.

Bi Mugabe aligonga vichwa vya habari mwaka ulopita alipoingoza kampeni ya kumfurusha aliyekuwa makamu wa rais bi Joice Mujuru kufuatia madai kuwa alikuwa ananuia kumpendua rais Mugabe.

Wakati huo alidhaniwa kuwa alikuwa anataka kumrithi mumewe lakini amejipata akijitetea katika siku za hivi punde kufuatia shinikizo la upinzani na visa kadhaa ambavyo rais Mugabe ameonekana kuwa mdhaifu wa siha.Image copyrightAPTNImage captionWapinzani wa rais Mugabe wamekuwa wakimshambulia kufuatia tukio alipokunguwaa na kuanguka

Wapinzani wa rais Mugabe wamekuwa wakimshambulia kufuatia matukio kadhaa ambayo amekunguwaa na kuanguka wengi wakimshawishi aachie madaraka kwani umri wake umezidi kuwa mkubwa na anapaswa kulegeza kamba.

Wapinzani wake wananukuu kisa alichosoma taarifa isiyofaa wakati wa ufunguzi wa kikao cha bunge.

Robert Mugabe ndiye rais mwenye umri mkubwa zaidi barani Afrika na amekuwa akiiongoza Zimbabwe tangu ijinyakulie uhuru wake mwaka wa 1980.

Uchaguzi mkuu ujao nchini Zimbabwe umeratibiwa kufanyika mwaka wa 2018.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake