Monday, November 23, 2015

Obama asema huwa hapaki nywele zake rangi


Obama aliingia mamlakani akiwa na nywele nyeusi 2009

Rais wa Marekani Barack Obama amesema yeye huwa hapaki rangi nyele zake kuficha mvi kama viongozi wengine duniani.
Kiongozi huyo wa umri wa miaka 54 alikuwa akimjibu mwanafunzi mmoja kutoka Cambodia aliyekuwa amemuomba ushauri wa busara.
Bw Obama aliingia mamlakani 2009 akiwa na nywele nyeusi lakini miaka ilivyosonga ameanza kuwa na mvi nyingi.
Rangi ya nywele za rais huwa suala tata wakati mwingine, na viongozi wengi wamekuwa wakificha ukweli kwamba hupaka rangi nywele zao.

"Jambo la kwanza ninalotaka vijana wakome kufanya ni kuniita mzee,” rais huyo alimwambia mwanafunzi huyo.
"Huwa sipaki nywele zangu rangi, na viongozi wengi duniani hufanya hivyo (kupaka nywele rangi),” alisema. "Sitasema ni kina nani. Lakini vionyozi wao wanawajua, na wasusi pia”.

Rais Ronald Reagan, kwa mfano hakuwahi kukiri kwamba alizoea kupaka rangi nywele zake, na kinyozi wake pia hakufichua hilo.

Chansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schroeder wakati mmoja alishtaki shirika la habari kwa kudai kwamba yeye alikuwa akipaka rangi nywele zake.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake