Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake, Rais Jakaya Kikwete ni kiongozi ambaye kwenye vitu atakavyokumbukwa kwa kuvifanya wakati wote wa uongozi wake ni juhudi zake kwenye kuinua Michezo TZ.
Ili Tanzania ifanye vizuri kwenye michezo kazi kubwa bado inatakiwa kufanyika, kinyume cha hapo hakuna miujiza itakayokuja kubadili hali na kuipandisha zaidi michezo.
October 17 2015 Rais JK alizindua Kituo maalum cha kukuza vipaji vya watoto kilichojengwa katikati ya Jiji Dar es Salaam eneo la Kidongo Chekundu… hiyo ni hatua nyingine nzuri kwamba uwekezaji wa vipaji unatakiwa kuanzia kwenye ngazi ya watoto.
Kama hujabahatika kupaona, unaweza kucheki hizi pichaz Kituo cha Michezo Kidongo Chekundu kwenye ubora wake yani.
Kwenye Kituo hicho watoto wanajifunza michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa miguu, Basketball na Volleyball.
Tangazo muhimu Kituoni.. Ni MARUFUKU kuvuta.
Huu ni Uwanja wa Mpira wa miguu.
Watazamaji wa game ya mpira wanaenjoy kila kitu wakiwa wamekaa hapo.
Muonekano mwingine wa viwanja ndani ya Kituo hicho huu hapa
Wale wa Basketball ??!! YES, hapo ndio penyewe.
Usafi ni muhimu kiukweli… Ndoo za taka zipo kuhakikisha hilo.
Ikitokea dharura ya moto, Fire extinguishers zimeandaliwa kabisa
Sehemu ya Ofisi za Kituo hicho ndio hizi mtu wangu.
Hivi ni vyoo
Hili ndio jina la Kituo hicho.
Ulinzi wa kutosha kwenye geti la kuingia ndani ya viwanja hivyo.
Ili usipotee, kuna kibao pia kinakuelekeza ndani kulivyo.Source:MillardAyo
No comments:
Post a Comment