Sunday, November 1, 2015

PINDA AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI NYUKI TANZANIA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ufugaji nyuki na usindikaji asali, Bw. David Kaizilegi Kamala (kushoto) katika maonyesho ya ufugaji nyuki na usindikaji asali yaliyotangulia uzinduzi wa Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania alioufanya kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha uanzishwaji wa Chama hicho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Parseko Konne. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Celestine Gesimba na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sabuni, mafuta na vipodozi vinavyotengenezwa kwa kutumia mazao ya nyuki kaba ya kuzindua Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
Waziri Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake