ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 1, 2015

Wachunguzi wa Urusi wawasili Misri

Kundi la wachunguzi wa Urusi wamewasili nchini Misri kubaini ni kitu gani kilisabasisha kuanguka kwa ndege ya Urusi katika rasi ya peninsula siku ya Jumamosi ambapo watu wote 224 waliokuwa ndani waliuawa.

Maaafisa nchini Misri na Urusi wamekana madai kutoka kwa kundi la Islamic State kuwa ndilo liliangusha ndege hiyo

Waziri mkuu nchini Misri Sherif Ismail alisema kuwa tatizo la kiufundi huenda ndilo lilisabaisha kuanguka kwa ndege hiyo.

Vinasa sauti vyote vye ndege hiyo vimepatikana na vitakaguliwa na wachungzui wa Urusi.

Licha ya matamshi hayo mashirika ya ndege ya Emirates, Air France na Lufthansa yamesitisha safari zao katika anga ya Sinai hadi pale habari zaidi zitakapotolewa.

BBC

1 comment:

Anonymous said...

poleni sana raia na wananchi wa urusi.mimi ni mtaalamu wa masuala ya anga.hii ndege iliyoanguka na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 220,ni moja ya ndege zilizo na ubora wa hali ya juu duniani.AIRBUS A321-200.umri wake tangu ilipotengenezwa wa miaka 18 ni umri mdogo na wa kawaida kwa viwango vya juu vya usalama wa ndege kufanya kazi.marubani wake kutoka urusi ni marubani wenye vipaji vya juu sana kurusha ndege duniani.na,sio ndege tuu bali hata vyombo vya kwenda sayari nyingine [mnamkumbuka marehemu yuri gagalin?].mrusi rubani ni makini,ni shupavu,ametulia nimwelewa mkubwa wa anga.hapa nilichogundua marubani wale[walikuwepo wawili]waliporuka na kuiingiza ndege kwenye cruising speed-futi 32,000 usawa wa bahari-waligundua hitilafu kubwa zilizojitokeza katika mitambo,wakatoa taarifa kwa waongozaji ndege waliopo ardhini,wakaomba ruhusa kuishusha nege hii kwa dharura,na ndipo ajali hii mbaya ikatokea. binadamu tunajifunza,kilichoumbwa na mwanadamu hakitokosa kasoro.poleni sana raia wa urusi,tunaipenda nchi yenu.