Kilimanjaro Lager imeendesha shindano hilo mara mbili ambazo zote Simba imekuwa ikiibuka kidedea kwa kuifunga Yanga, mwaka juzi Simba ilishinda mabao 3-1 wakati mwaka jana walishinda 2-0.
Meneja wa kinywaji hicho, Pamela Kikuli aliliambia Mwanaspoti kuwa wamekuwa wakifanya shindano hilo kwa mafanikio kipindi chote lakini mwaka huu hawataweza kuendesha shindano hilo kwani halipo kwenye mikataba yao na timu hizo.
Alisema walishakaa na viongozi wa pande zote mbili na kuwapa taarifa za awali kuwa huenda mwaka huu lisiwepo ama liwepo hivyo wajiandae kwa lolote.
“Wanajua hilo japokuwa hatujawaambia kiofisi, tulikaa nao awali ambapo tuliwaambia kuwa tunaweza kufanya ama tusifanye. Endapo tungefanya basi tungekuwa tumeanza kufanya matangazo yetu lakini kiukweli hatutafanya na hatuoni sababu ya kuwaambia kwani wana taarifa za awali.
“Sababu kubwa za kutofanya mwaka huu ni za ndani ya kampumni yetu hivyo zinabaki kuwa ndani kwasababu shindano hili ni kama kufanya promosheni tu kwa timu hizo kwani halipo kwenye mikataba yetu ya udhamini kwao,” alisema Pamela.
Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amesema kuwa “Tulipata taarifa hizo muda mrefu na hazijatuathiri chochote kwani lilikuwa ni bonanza tu japokuwa lilikuwa zuri kwa kutukutanisha na watani zetu, ingawa hatukuambiwa sababu za msingi za kufutwa kwa shindano hilo.”
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment