Advertisements

Friday, December 11, 2015

Paul Makonda azindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka Global

Shinda Nyumba na Global (11)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd. Kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo.
Shinda Nyumba na Global (12)
Shinda Nyumba na Global (13)
Paul Makonda akigawa vipeperushi vyenye nyumba na zawadi nyingine zinazoshindaniwa kwa wanahabari.

Shinda Nyumba na Global (1)
Shinda Nyumba na Global (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akiwakaribisha wanahabari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda katika uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba uliofanyika katika ofisi za Global zilizopo Mwenge, Bamaga jijini Dar. Shinda Nyumba na Global (3) Shinda Nyumba na Global (4)
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio.
Shinda Nyumba na Global (5)
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo akiongea na wanahabari kuhusu lengo la Global kuendesha shindano hilo.
Shinda Nyumba na Global (6)
Shinda Nyumba na Global (9)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka Global.
Shinda Nyumba na Global (7) Shinda Nyumba na Global (8)
Wanahabari wakimsikiliza Paul Makonda.
Shinda Nyumba na Global (10)
Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akimkaribisha Paul Makonda (katikati) kuzindua rasmi Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers. Wengine pichani ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Oscar Ndauka (wa kwanza kulia), Mhariri Mtendaji wa Global Richard Manyota (wa kwanza kushoto) na Eric Shigongo wa pili kushoto.
Shinda Nyumba na Global (14)
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika picha ya pamoja na Paul Makonda mara baada ya uzinduzi huo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WASOMAJI WA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS KUJISHINDIA NYUMBA, PIKIPIKI, TV NA ZAWADI NYINGINE NYINGI
KAMPUNI ya Global Publishers Ltd inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda yanayosambazwa nchi nzima, imeandaa Bahati Nasibu kwa wasomaji wa magazeti yake ambayo inaanza rasmi Ijumaa, Desemba 11, 2015. JINSI YA KUSHIRIKI Msomaji atatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti tajwa na kukata kuponi moja iliyomo ndani ya magazeti hayo. Atatakiwa kujaza jina lake kamili na anwani yake na kisha kuituma kwa njia ya posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers au kwa mawakala wake waliyopo sehemu mbalimbali nchini. Kwa wale wa mikoani, nao wanaweza kutuma moja kwa moja kwa mawakala wetu au kutuma kwetu kwa njia ya posta. Kutakuwa na vituo vya kukusanyia kuponi katika kila kata na mitaa mbalimbali nchini Tanzania. ZAWADI Bahati Nasibu hii inatarajiwa kuendeshwa kwa muda wa miezi 6, tunatarajia kutoa zawadi ya nyumba mpya mwishoni mwa mchezo huu ambayo imejengwa eneo la Salasala, Wilayani Kinondoni, jijini Dar es salaam, nyumba hiyo ni mpya kabisa na itakuwa na samani ndani na hadi sasa imeshamilika kwa alilimia 95. Pia kutakuwa na Droo nyingine ndogo kila mwezi zitakazotoa zawadi za Simu za Kisasa, Runinga na Ving’amuzi vyake, na vyombo vya mbalimbali vya nyumbani. MASHARTI Wasomaji wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanaruhusiwa kushiriki, lakini wafanyakazi wa Global Publishers, waandishi wake na ndugu zao hawaruhusiwi kushiriki. Msomaji anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi ya Nyumba na zawadi nyingine. Kuponi zote zitaingia katika droo ndogo na kubwa. HISTORIA YA GLOBAL KATIKA BAHATI NASIBU GLOBAL Publishers ni kampuni pekee ya uchapishaji wa magazeti nchini ambayo imekuwa ikiandaa Bahati Nasibu na kutoa zawadi kubwa kwa wasomaji wake mara kwa mara. Imekuwa ikiendesha Bahati Nasibu mbalimbali kupitia magazeti yake tangu mwaka 2000 na kwa nyakati tofauti imeshatoa jumla ya magari 5, kama vile Nissan March, Toyota Vitz, Mitubish Pajero, Mercedes Benz na Toyota Noah na zawadi nyingine nyingi za tahamani, ikiwemo kumpeleka msoamaji wake mmoja Hong Kong kutalii. Global Publishers imekuwa ikifanya yote haya si kwa sababu ina fedha nyingi sana, bali inafanya haya kama njia moja wapo ya kuwashukuru wasomaji wake kwa kuendelea kuyaamini na kuyasoma magazeti yake kwa zaidi ya miaka 15 sasa, pia inafanya haya kama njia moja wapo ya kurejesha kwa wasomaji sehemu ya kipato chake ili kuboresha maisha yao. Aidha inafanya hivi pia kwa ajili ya kuimarisha na kuongeza idadi ya wasomaji wake. Mwisho, tunawahakikishia wasomaji wetu kuwa washindi wote wa Bahati Nasibu za Global publishers hupatikana kihalali chini ya usimamizi madhubuti wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha na huchezeshwa kwa wazi kila mtu akiona. Tunakushukuru sana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda kwa kuja kuizindua rasmi Bahati Nasibu hii na tunakupongeza kwa kazi yako nzuri kwa taifa. Asante Meneja Mkuu, Global Publishers Ltd.

No comments: