Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika katika Tume ya Mipango. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri.
Mmoja ya watumishi wa Tume ya Mipango Bw. Mohamed Ally akiongea mawili matatu na waziri mara baada ya mkutano kuisha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na watumishi wa Tume ya Mipango alipowatembelea kwa kusudi la kuwaaga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameiagiza Tume ya Mipango kufanya utafiti kuhusu mapato ya Serikali na namna ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.
Amesema Tume ya Mipango kama chombo cha ushauri kwa Serikali kuhusu mipango na uchumi wa nchi, ni lazima ifanye utafiti juu ya ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuongeza vyanzo wa kukusanya mapato ya Serikali ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi wake.
“Serikali isipokusanya kodi kwa ufanisi haiwezi kuwahudumia wananchi hivyo, ni lazima kodi ikusanywe ipasavyo ili kuiwezesha kujiendesha” alisema.
Dkt Mpango aliyasema hayo alipokutana na wafanyakazi wa Tume ya Mipango kwa lengo la kuwaaga baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Waziri wa Fedha amesema mianya yote ya ukwepaji kodi ni lazima izibwe ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato ya kutosha suala ambalo litairahisishia utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.
Amesema Serikali haiwezi kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili wakati nchi ina rasilimali za kutosha hivyo.
Dkt. Mpango amesema Tume ya Mipango ni lazima iongoze nchi kuelekea katika uchumi wa viwanda ambavyo vitafanya pato la taifa kuongezeka na kutoa ajira kwa wananchi.
“Sisi kama wataalamu tunatakiwa kuiongoza nchi katika kufikia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 jambo ambalo linawezekana” alisema.
Waziri pia amesema ni lazima tujenge uchumi imara na madhubuti utakaowezesha kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.
“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuboresha ufanisi na utendaji wa Serikali kwa ujumla hivyo ninyi kama wataalamu mna mchango mkubwa katika kutimiza hilo” alisema.
Tume ya Mipango ni chombo mahususi cha fikra rejea na ushauri kwa serikali kuhusu sera na mikakati ya maendeleo, kiuchumi na kijamii ambao unaambatana na ufuatiliaji na utathmini wa mwenendo wa uchumi nchini.
Aliwataka wafanyakazi wa Tume ya Mipango kufanyakazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa ili kuimarisha utendaji Serikalini.
No comments:
Post a Comment