ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 16, 2016

I WAS LOST, VIDEO MPYA YA ROSE KACHUCHURU Rose Kachuchuru ni dada anaeishi katika jimbo la Maryland nchini Marekani akijishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtukuza Mungu kwa nyimbo za injili. Rose ambae ni mama wa watoto wawili Mathew Baraka na Marina Zawadi amekuwa akijishughulisha na kazi hii ya uimbaji wa nyimbo za injili kwa Muda sasa akiwa ni zao la kikundi cha nyimbo za injili cha kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries kilichoko Washington DC kwa sasa, ambako huko alikuwa ni mmoja wa waimbaji mahiri. Akiongea na mwandishi Rose alieleza ni kwa namna gani amefika hapo alipo sasa, yafuatayo ni maneno yake mwenyewe..... "Mimi kwa jina naitwa Rose Kachuchuru. Nimetoka kwenye familia ambayo inamcha Mungu sana. Wazazi wangu walikuwa ni wacha Mungu wa kweli. Baba yangu alikuwa anampenda sana Mungu. Yeye alikuwa analala kanisani siku za sikukuu kama Christimas na Pasaka. Alikuwa ni muombaji sana. Wazungu huwa wanawaita Prayer warriors. He was one of those people. Japokuwa nilitoka katika familia ya kumcha na kumpenda Mungu sana mimi kiukweli nikiangalia nyuma sasa naona sikuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Enzi hizo mimi nilidhani kwenda kanisani kila siku ilikuwa inatosha kabisa. Sikujuwa kwamba kuna mambo mengi nilitakiwa niyajue na kuyafanya. Ninaposema sikuwa na uhusiano mzuri na Mungu namaanisha sikumjuwa Mungu kama ilivyotakiwa nimjuwe Mungu. Ninavyomjuwa Mungu leo ni tofauti na nilivyokuwa namjuwa zamani. Leo nimeona matendo yake mengi ya ajabu katika maisha yangu. Nimeyaona haya yote pale tu nilipoamua kuwa na uhusiano mzuri na yeye. Nikirudi nyuma kidogo nikupe tu historia fupi ya kwangu. Mimi tangu nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda saana kuimba. Nakumbuka usiku nyumbani kwetu tulikuwa tunaimba sana nyimbo za tenzi za rohoni. Nanilipoanza shule ya msingi nilikuwa katika band na kwaya ya shule. Pia hata kanisani nilijiunga na kwaya za kanisani. Nakumbuka nilipokwenda secondary school niliendelea kuimba mpaka kuna kipindi nilitunga wimbo na tukaenda kushindana na shule zingine za mikoa na tukashinda. Wakati huo mimi sikuona kama ni kitu kikubwa sana nimefanya. Na hata wengine pia sidhani waliona ni kitu kikubwa. Kama tunavyojuwa familia nyingi za kiafrika hazithamini vitu kama hivyo. wazazi wengi wa kiafrika wanapenda watoto wao wawe Madaktari, Ma lawyer au Ma judges. Mambo ya kuimba huona ni upuuzi tu. Nikiwa hapa Marekani mwaka 2008 nilijiunga na kanisa linaloitwa The way of the Cross Gospel Ministries. Mimi nilikuwa mmoja wa wanzilishi wa kanisa hilo. Wakati nikiwa kwenye kanisa hilo tuliunda kikundi cha kuimba ambacho sasa kinaitwa The Sound of Glory Singers. Mara nyingi nilpokuwa nikipata nafasi za kuimba mwenyewe watu wengi walikuwa wakija na kuniambia nimewagusa roho zao na nimewabariki sana katika uimbaji wangu. Hiyo ilinipa motisha kubwa sana. Nikasema labda Mungu anataka nimuimbie. Wengi walinisisitiza sana kwamba nina kipaji cha kuimba. Wengine waliniambia nipige magoti nimuombe Mungu aniongoze katika hili. Na mimi nilichukuwa ushauri wa watu hao nikaanza kumuomba mungu anipe direction na kwakweli nilianza kumuona mungu aniongoze katika kumuimbia yeye. Niliamua kuondoka The Way of the Cross Gospel Ministries na nikaanza kuconcentrate na kutengeza nyimbo za kumtukuza na kumsifu bwana. Nilipitia majaribu makubwa sana wakati huo mpaka nikawa sielewi ni kwanini? Niliamua kumuuliza Mungu ni kwa nini anaruhusu mapigo mazito namna hiyo yanifuate baada ya mimi kuamua kumtumikia kwa kumwimbia. Kiukweli mimi sikujuwa kuwa unapoamua kumtumikia Mungu kwa kumsifu shetani atakuandama ili uache. Mapigo yalikuwa makubwa sana. Lakini Mungu kwa rehema na neema yake aliniona na akanipigania. Kuna wimbo wangu mmoja unaitwa I was lost (tazama video juu0, huu ni wimbo ambao unamaana kubwa sana katika maisha yangu. Niliandika huu wimbo kuhusu jinsi nilivyokuwa nimepotea sikujuwa nilipokuwa nakwenda na sikujua maisha yangu yatakuwaje baadae. Nilianza kumlilia Mungu sana nikasema napenda kuwa na mahusiano Mazuri na yeye. Hapo tu nilipoamua kumkabidhi yeye maisha yangu yote, ni hapo ndipo nilipoanza kuona mabadiliko mengi sana katika maisha yangu. Nimeona jinsi gani Mungu ananipenda sana, ananitakia mema siku zote na jinsi gani hawezi kuniacha niangamie. Sikuweza kuyaona haya yote kwasababu nilikuwa nimefungwa lakini Mungu sasa amenifungua na naweza kuyaona makuu yake mengi katika maisha yangu. Yeye ni kimbilio langu, mwamba wangu, na yeye ni kila kitu katika maisha yangu. Nimempata yeye siwezi kumuacha kamwe. Ushauri wangu kwa wale wote wanaomjua Mungu na kumwabudu. Wamkabidhi yeye pekee maisha yao yote, wafanyapo hivyo tu watayaona makuu na matendo yake ya ajabu katika maisha yao. Yeye atawapigania, atawalinda, atawatendea mema na hatawaacha waangamie kamwe. Mungu ni mwema siku zote”. div dir="ltr" style="text-align: left;" trbidi="on">

No comments: