Na Mwandishi wetu,
Matibabu
ya kawaida ya saratani huwa yanahusisha upasuaji, radiotherapia na
kemotherapia. Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa kwenye tiba kwa njia
hizo mbili. Katika hatua za mwanzo, saratani huwa ni ugonjwa unaotibika kwa
dozi moja mahususi lakini saratani iliyosambaa au kukomaa inahitaji dozi zaidi
ya moja katika kuitibu. Radiotherapia, ni tiba iliyopo katika mfumo maalumu
unaoleta matokeo katika mwili mzima.
Dk.
Mahadev ,
mshauri mwandamizi wa tiba ya uvimbe kwa mionzi kutoka hospitali za Apollo
anaeleza kwamba radiotherapia inahusisha chembe chembe ndogo za mionzi ya gamma
au X-rays katika kutibu saratani na hata matatizo ambayo sio ya saratani pia.
Mionzi hii imegawanyika katika ile mionzi ya mbali (external radiotherapy)
ambayo chanzo cha mionzi kinakuwa mbali na mwili na ile mionzi ya karibu ambayo
mionzi inawekwa karibu ili kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake.
Mionzi
ya karibu ni aina nzuri ya kutibu saratani ila kwa uvimbe unaoonekana kirahisi
na unaofikika. Hivyo saratani iliyopo mdomoni, saratani ya tezi dume, saratani
ya kizazi zote zinaweza kutibiwa kwa mionzi ya karibu peke yake. Faida kubwa ya
mionzi ya karibu ukilinganisha na mionzi ya mbali ni kwamba mionzi ya karibu
inahusisha uponyaji ndani ya muda mfupi (siku 3-5) wakati mionzi ya mbali
inachukua hadi wiki 7 hadi 8. Uvimbe wowote uliokomaa unahitaji mionzi ya
mbali.
Lengo
kubwa la matumizi ya radiotherapia ni kuchoma sehemu pekee yenye uvimbe na
kuepuka kuchoma sehemu nyingine za pembeni katika mwili. Mionzi ya mbali
inahistoria ndefu kutoka enzi za cobalt kwenda kwenye hali ya teknolojia ya juu
ya kutoa tiba ya mionzi kwa moduli ya hali ya juu (IMRT), mionzi kwa kuongozwa
na picha (IGRT), upasuaji kwa njia ya sterio (SRS) na njia ya sterio kwa mionzi
mwilini (SBRT). Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji (Cyberknife
robotic radiosurgery ) ni njia bora zaidi katika kufanya SRS na SBRT,
aliongeza Dk. Mahadev kuwa teknolojia hizi zinapatikana
katika hospitali za Apollo.
Umuhimu
pekee wa kutumia mashine yenye program maalumu kwa ajili ya upasuaji ni kukata
milimeta sahihi na uponyaji katika siku chache. Ni tiba ya mgonjwa bila kulazwa
na hahihitaji nusu kaputi katika kufanyika. Hivyo saratani ya mapafu na tezi
dume inaweza kutibika ndani ya siku 3 hadi 5, wakati muda wake kawaida huchukua
wiki 7-8 kwa uangalizi wa karibu. Mashine yenye program maalumu kwa ajili ya
upasuaji ni muhimu katika kutibu uvimbe, ambao hauwezekani kufanyiwa operesheni
kwa sababu ya eneo ilipo aidha katika ubongo au uti wa mgongo. Inatumika kutibu
magonjwa kama meningiomas, uvimbe katika pituitary, mishipa ya ateri
iliyodhofika (AVM) na madhara kutokana na saratani katika ubongo, mapafu na
ini.
Dk.
Mahadev
anaelezea njia bora ya kutumia radiotherapia ni kwa protoni. Faida kubwa ya
protoni ukilinganisha na njia ya kawaida ni katika kutoa mionzi kwa umakini
zaidi hasa kuchoma sehemu yenye uvimbe peke yake. Hiyo inapelekea matokeo
mazuri na madhaifu machache. Kutokana na kutokuwa na dozi zaidi katika kutibu
uvimbe, ni vyema kudhibiti uvimbe ukiwa katika hatua za mwanzo ambapo huwa
tunaogopaga madhara ya kutumia mionzi. Matumizi ya protoni ni mapinduzi katika
tiba ya saratani. Saratani ya kichwa na shingo, mapafu na tezi dume huwa
zinatibika kirahisi kabisa kwa mionzi hii ya protoni.
Baadhi
ya saratani zinazotibika kwa upasuaji, inaweza kutibika kirahisi kwa
radiotherapia tu. Ikiwa hatua ya mwanzo, saratani ya mdomoni, mfumo wa chakula,
tezi dume, zaweza tibiwa kwa mionzi peke yake. Faida katika kutibu aina hizi za
saratani ni kuwa zipo sehemu zinazofikika. Mgonjwa anaweza kuwa na ogani
inayofanya kazi vizuri hivyo kuona ubora wa maisha. Saratani nyingi zilizokomaa
huwa zinahitaji kwa pamoja upasuaji, radiotherapia na kemotherapia katika
kuitibu ambazo zote zinapatikana katika teknolojia ya juu kutoka hospitali
za Apollo.
Tumetoka
kwenye enzi za kufanya operesheni kubwa na kuingia kwenye utunzaji wa ogani
zetu kwa msaada wa teknolojia ya mionzi bora na dawa mpya na bora za tiba kwa
kemotherapia. Kwa mfano saratani ya matiti ndio saratani inayoongoza kwa
wanawake duniani. Hapo kabla, titi lote lilikuwa linakatwa. Ila kwa sasa
wagonjwa wengi wanabaki na matiti yao salama kwa upasuaji mdogo tu unaofanywa.
Tiba
hiyo ndogo katika tiba inawasaidia wanawake kuwa na saikolojia chanya
inayowafanya wapone haraka pia. Kichwa na shingo, mfumo wa chakula, saratani ya
tezi dume na sehemu nyingine ambazo huwa kutokuondoa ogani ni kitu cha muhimu
katika tiba.
Radiotherapia
ni mbadaka zuri kuepuka upasuaji au kemotherapia katika kupambana na saratani.
Mabadiliko makubwa katika teknolojia na matumizi ya kompyuta yamewezesha utoaji
bora wa huduma ya tiba ya mionzi kwa madhara kidogo sana.
Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali za Apollo ni za kwanza
katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa
Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji
kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma
bora kwa wagonjwa.
Taasisi ina wataalamu waliobobea
kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu
vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na
vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.
Mfumo
huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa
yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology),
moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.
No comments:
Post a Comment