ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 14, 2016

MKUU WA WILAYA YA IRINGA MHE RICHARD KASESELA AONGOZA ZOEZI LA UOKOAJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO KIJIJI CHA PAWAGA

kitongoji cha Nyalu wamezingirwa na maji
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa zimesomba mashamba na nyumba na kuwaacha wananchi wengi wakiwa hawana mahali pa kukaa. 
Vitongoji vilivyo athirika sana ni Kisanga, Nyallu, Makoka na Mbughani. Mpaka sasa bado idadi isiyo rasmi inakadiliwa watu zaidi ya 200 bado wamezingirwa na maji siku ya 4. 
Juhudi za uokoaji zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela zimefanikiwa kuokoa watu 399 kitongoji cha Kisinga, watu 38 kutoka kitongoji cha Makoka, na watu 23 kutoka kitongoji cha Nyalu. Jeshi la polisi lilitoa helicopter kusaidia uokoaji na pia kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa mstari wa mbele kwenye zoezi hilo. 

Maeneo mengi yalihitaji waogoleaji mahiri ili kuwafikia wananchi. Zoezi linaendelea hado sasa. shule 2 zimetengwa kwa ajili ya kupokea wahanga wa mafuriko shule ya msingi Itunundu na shule ya msingi Kisanga.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongoza uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la  uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la  uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Eneo lililoathirika
Njia haipitiki kwa vyombo vya moto



Familia zikiwa imezingirwa na maji

3 comments:

Anonymous said...

tuna uhuru wetu tuna nchi yetu tuna rasilimali zetu hivi kwanini hali kama hivi zinatokea au tunamsubiri mzungu aje atutawale tena. ni bora aje atutawale tena.

Anonymous said...

Mafuriko hutokea na kuleta madhara kila mahali,iwe first world or third world.

Anonymous said...

Haya mafuriko ni ya kila mwaka. Ngojea mvua ziishe na watu watarejea huko huko. Hichi ndicho tunachokidhania kuwa ni cha ujinga!
Kila mwaka kinatokea na kila mwaka kinarejea nasi hatuhami hata kidogo, kwanini? Kuna mizimu yetu huko mabondeni????