ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 15, 2016

DKT. KIGWANGALLA AZIFUNGIA HOSPITALI MBILI ZA KIGENI

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamis Kigwangalla amezifungia hospital mbili tofauti zinazomilikiwa na Raia wa kigeni wakiwemo kutoka Korea kwa kile walichoeleza kuendesha huduma bila vibali maalum ikiwemo usajiri wa msajili wa hospital binafsi pamoja na ule wa msajili wa tiba mbadala.

Miongoni mwa vifaa vilivyokutwa ni pamoja na vile vinavyotumika mahospitalini na vingine vile ambavyo hawakuruhusiwa.
Hospitali hizo zilizovamiwa na kukaguliwa ni pamoja na Korea Medical Clinic ya Kariakoo Mtaa wa Mahiwa na nyingine ni Oriental Traditional medicine clinic... Ambazo zote zinazomilikiwa na Mabong.

Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa watu hao wamekuwa wakitoa huduma bila vibali halali huku pia wakiendesha huduma pasipo kufahamu lugha za kiswahili na Kiingereza.

1 comment:

Anonymous said...

PAMOJA NA NAIBU WAZIRI KUFUNGIA HOSPITALI HIZI, ITAKUWA JAMBO LA MSINGI KAMA TUTAJIULIZA HUYU NAIBU WAZIRI ATAFUNGIA HOSPITALI NGAPI KAMA HIZI. KWA KIFUPI BADO SIO KAZI YA WAZIRI KUZUNGUKA LI-NCHI LOTE HILI KUTAFUTA HOSPITALI ZENYE MATATIZO WAKATI KUNA OFISI STAHIKI ZA KUFANYA KAZI HIZO. KWA MANTIKI NYINGINE HII NI DALILI TOSHA YA KUWA BADALA YA KUWA NA MFUMO THABITI WA AFYA, BADO TUNATEGEMEA MTU MMOJA MMOJA. DR. KINGWALLA, HILI LA MFUMO NI WAJIBU WAKO, YAANI WEWE, WAZIRI WA AFYA PAMOJA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA, BADALA YA KUFANYA HIVI MNAVYOFANYA, NI VYEMA MKATENGENEZA SERA NA SHERIA THABITI (KAMA HAZIPO) KUSIMAMIA HAYA. NA KAMA SERA NA SHERIA ZIPO, BASI WAHUSIKA KATIKA WILAYA NA MIKOA WANA WAJIBU WA KUZITUMIA. VINGINEVYO HIZI ZOTE NI ALFU ULELA ULELA...