Dar es Salaam . Mawaziri wawili wenye dhamana ya afya na ufugaji, Ummy Mwalimu na Mwigulu Nchemba, wameruhusu machinjio ya Vingunguti kufanya kazi kwa muda kuanzia leo usiku ili kukidhi haja ya upatikanaji nyama.
Hatua hiyo imekuja baada ya mawaziri hapo kutembelea eneo hilo, ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja tangu wafungie machinjio hayo kwa kutofuata kanuni za kiafya.
Hata hivyo, wameshangazwa na kasi ndogo ya ukarabati wa miundombinu ya machinjio hayo tangu ilipofungwa ili kuiboresha kabla ya kuendelea na kazi.
Waziri Ummy amesema kuwa wameagiza uongozi wa machinjio hayo wahakikishe kuwa wanarekebisha baadha ya miundombinu muhimu kufikia leo jioni ili usiku shughuli za uchinjaji uanze, hata hivyo machinjio yatafungwa tena kwa siku tatu kuanzia Jumanne ili kuruhusu ukarabati mkubwa
No comments:
Post a Comment