ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 18, 2016

MAWAZIRI WAFUNGUA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

f8dfac6d-dae1-44c2-8ffa-fc6be60449e0
Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Isaya Mgulumi (mwenye miwani) akiwaeleza mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati) na Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mwigulu Nchemba (kushoto) akiwaelezea hali ya ukarabati wa machinjio hayo.
aa171e5b-ad5c-410d-be1b-a7c004dbf0f7
Mkaguzi toka TFDA Dkt. Mwanga Itikija (mwenye shati la pink) akiwaonesha mawaziri hao eneo ambalo lilikua likiuzia nyama kwa reja reja kinyume na kanuni ya afya.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba kwa pamoja na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wametembelea machinjio ya Vingunguti na kuona jinsi hali ilivyo katika eneo hilo.
Pamoja na kutembelea eneo hilo ambalo lilikuwa limefungiwa kuchinja nyama, mawaziri hao wameruhusu kwa siku tatu kuchinja huku wakitoa maagizo kwa Halmshauri ya Manispaa ya Ilala kuhakikisha wanapafanyia marekebisho.
739650f0-4eb7-481c-84b2-d8ac352faaa4
Baadhi ya wafanyabiashara wa machinjio hayo wakifuatilia ziara hiyo.
5b8c1806-59ea-4587-b885-955346eb9298
Mbunge wa jimbo la Segerea, Bona Kalua, akiongea na wanachama wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Ng'ombe na mazao yake (UWAMI) kwenye mkutano wa pamoja na mawaziri hao.
e8a001c5-d042-4f34-acc9-dfae21d50c7f
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Wanachama wa umoja huo, ambapo aliwasisitiza kufanya biashara kwa kuzingatia kanuni za afya na kumlinda mlaji hivyo kuwa makini na utunzaji wa mazingira pamoja na mazao wanayoyauza machinjioni hapo.
216ecacf-c7ac-4930-8af2-2bf5770afc8a
Waziri Mwigulu Nchemba akiongea na Umoja huo na kuwapatia siku tatu ili waendelee na uchinjaji wa ng'ombe walizonazo na baada ya hapo wataendelea na ukarabati wakati huo machinjio ya mazizini yatakua yamekamilisha ukarabati na kufunguliwa.
b747d339-237d-4c7f-997c-bf5c30323ea8
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilaya ambaye ndio Diwani wa kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto akiongea kwenye mkutano huo.
dd1803c0-1811-4f98-bf71-78c255242dd4
Mawaziri wakisoma vielelezo vilivyowasilishwa na diwani wa kata hiyo.
806aba0d-2e1e-4a49-933d-6e032ef06ee7
Wanachama wa Umoja wa wafanyabiashara hao waliwasikikiliza mawaziri hao (Picha na Wizara ya Afya)

No comments: