Na David John, Mkuranga.
MBUNGE wa Jumbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega amekabidhi jezi seti20 na mipira 20 zenye thamani ya sh.milioni 4katika shule zote za Sekondari zilizopo katika Jimboni hapa.
Akikabidhi jezi hizo wilayani hapa jana katika hafla fupi iliyowakutanisha walimuwakuu, wanamichezo, watendaji wa halmashauri ,pamoja na Ofisa Elimu ,Ulega amesema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
"Ndugu zangu walimu na manahodha wa timu zote Kutoka shule 20 za sekondari zilizoponda ndani ya Jumbo langu la Mkuranga nimetoa vifaa hivi ili muweze kushiriki vyema katika michezo ya shule za Sekondari UMISETA nakutuletea mafanikio,"alisem Ulega.
Pia amesema kuwa anatambua kuwa kuna changamoto za kutosha katika michezo hususani vifaa vya michezo Kwa kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo huku akiwataka wanafunzi na walimu hao kusimamia vyema.
Aidha Mbunge Ulega amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati Kwa walimu na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo ili Kwa pamoja kuharakisha maendeleo jimboni hapa ikiwamo michezo.Pia amewaambia viongozi hao kujenga mashirikiano ya Katibu na yeye kama mwakilishi wao yupo tayari Kwa wakati wowote kutumika na kusikiliza maoni yao.
Kwaupande wake Ofisa Elimu wa Halmashauri Kwa upande wa shule za Sekondari Benjamini Majoya akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa Mbunge Ulega amefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa Kwa viongozi wengine waliotangulia.Amesema kuwa watamuunga mkono Mbunge huyo Kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika nyanja ya Elimu na michezo Kwa ujumla.
"Kwanza tunashukuru Kwa vifaa hivi kwani vimekuja katika wakati muhimu ambapo tunakwenda katika mashindano ya UMISETA na Kwa vifaa hivi ushindi upo,"amesema Majoya.Pia ameongeza kuwa hakuna ubishi kwamba michezo ni ajira hivyo lazima watahakikisha vijana hao wanafanya vizuri katika michezo na taaluma pia.
1 comment:
Tatizo la wanasiasa kuwaharibu watanzania usihangaike elimu zao au kufungua academy mpira ili iwe ajira yao kila mwanasiasa anataka kutoa jezi nguo inavaliwa unatupa
Post a Comment